logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bei ya mafuta yapanda Tanzania

Ongezeko hilo la bei limechangiwa na kuongezeka kwa bei ya mafuta yaliosafishwa katika soko la dunia

image
na SAMUEL MAINA

Habari04 April 2024 - 05:39

Muhtasari


  • •Mamlaka ya udhibiti wa huduma ya Nishati na maji Ewura imesema ongezeko hilo la bei limechangiwa na kuongezeka kwa bei ya mafuta yaliosafishwa katika soko la dunia

Bei za mafuta nchini Tanzania zimepanda mwezi huu Aprili ikilinganishwa na mwezi Machi 2024.

Katika Jiji la Dar es Salaam mafuta ya petroli yamependa kutoka Tsh. 3,163  mwezi Machi hadi 3,257 kwa lita huku dizeli ikiongezeka kutoka Tsh. 3126 hadi 3,210 mwezi Aprili.

Mamlaka ya udhibiti wa huduma ya Nishati na maji Ewura imesema kwamba ongezeko hilo la bei limechangiwa na kuongezeka kwa bei ya mafuta yaliosafishwa katika soko la dunia, mbali na ongezeko la kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni kwa asilimia 3.19 kutokana na ongezeko la matumizi ya Euro kulipia mafuta yalioagizwa.

Bidhaa hiyo pia imeongezeka bei katika miji ya Tanga , na Mtwara ambako itauzwa kutoka Tsh. 3,209 hadi Tsh. 3,303.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved