Kifo cha balozi wa Urusi, Msumbiji yachunguza

Alexander Surikov, 68, alipatikana amekufa Jumamosi usiku katika makazi yake rasmi katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo.

Muhtasari

• Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wa Msumbiji imesema kuwa haikufahamu madai ya kukataa kwa mamlaka ya Urusi kufanya uchunguzi wa mwili.

Image: UBALOZI WA URUSI NCHINI MSUMBIJI

Serikali ya Msumbiji imesema inashirikiana na mamlaka mjini Moscow kuchunguzakifo cha Balozi wa Urusi Alexander Surikov.

Surikov, 68, alipatikana amekufa Jumamosi usiku katika makazi yake rasmi katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana.

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wa Msumbiji imesema kuwa haikufahamu madai ya kukataa kwa mamlaka ya Urusi kufanya uchunguzi wa mwili wa balozi huyo kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya ndani.

Katika taarifa, Rais Filipe Nyusi alisema kifo cha Surikov kiliacha "pengokubwa", akimtaja kama mwanadiplomasia aliyejitolea na sifa za kipekee, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Surikov aliteuliwa katika nafasi hiyo mnamo 2017.