Mama akiri kukatisha maisha ya mwanawe mwenye saratani

Amekiri kwamba alimpa mwanawe kipimo kikubwa cha "morphine" kukomesha mateso anayopitia.

Muhtasari

•Antonia Cooper alisema mwanawe alikuwa na saratani ya hatua ya nne na alikuwa katika "maumivu makali" kabla ya kufariki mwaka 1981.

•Kusaidia mtu kufariki dunia, au kumsaidia mtu mwingine kimakusudi kumaliza maisha yake ni kinyume cha sheria nchini Uingereza.

Image: BBC

Mama mmoja amekiri kwamba alimpa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka saba, ambaye alikuwa akiugua saratani, kipimo kikubwa cha "morphine" ili kukomesha mateso anayopitia na "kumaliza maisha yake kimya kimya."

Antonia Cooper, kutoka Abingdon, Oxfordshire, alisema mwanawe Hamish alikuwa na saratani ya hatua ya nne na alikuwa katika "maumivu makali" kabla ya kufariki mwaka 1981.

Mama huyo sasa anaugua saratani, kulingana na kile alichosema wakati wa mahojiano na BBC Radio huko Oxford, kama sehemu ya jaribio linalolenga kubadilisha sheria na kuruhusu "kusaidiwa kufariki dunia" kwa watu wanaoteseka.

Kusaidia mtu kufariki dunia, au kumsaidia mtu mwingine kimakusudi kumaliza maisha yake, ambayo pia huitwa "euthanasia" au "kumaliza maisha ya mtu kimakusudi", ni kinyume cha sheria nchini Uingereza.

Hali ya mtoto huyo iligunduliwa akiwa na umri wa miaka mitano, na awali madaktari walimwekea makataa ya miezi mitatu, lakini mama yake alisema kwamba baada ya miezi 16 ya matibabu ya saratani "ya kutisha" katika Hospitali ya Great Ormond Street, Hamish aliendelea kuishi lakini alianza kuteseka kwa maumivu makali.

Akaongeza: "Usiku mmoja aliposema ana maumivu makali, nilimwambia: Je! unataka nikuondolee maumivu haya? Akasema: Ndiyo, tafadhali, mama."

Anasema: "Nilimpa, kupitia Hickman catheter, dozi kubwa ya morphine, ambayo ilimaliza maisha yake kwa amani.