Keir Starmer atarajiwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza

Chama cha Labour kinakaribia kupata ushindi wa kishindo huku Conservative kikikabiliwa na hali mbaya zaidi.

Muhtasari

•Sir Keir Starmer anaelekea Downing Street akiwa na idadi kubwa ya wabunge 160, kulingana na makadirio ya BBC na viti zaidi ya 160 vilivyotangazwa.

Image: BBC

Chama cha Labour kinakaribia kupata ushindi wa kishindo huku Conservative kikikabiliwa na hali mbaya zaidi katika uchaguzi mkuu kuwahi kushuhudiwa, matokeo ya awali yanaashiria.

Sir Keir Starmer anaelekea Downing Street akiwa na idadi kubwa ya wabunge 160, kulingana na makadirio ya BBC na viti zaidi ya 160 vilivyotangazwa, vichache kiasi kuliko ilivyotabiriwa na kura ya maoni.

Katika hotuba yake ya ushindi wa eneo bunge, kiongozi huyo wa chama cha Labour alisema ni "wakati wa sisi kutoa".

Conservertive wanatabiriwa kuishia na wabunge 154, idadi ya juu kidogo kuliko ilivyotabiriwa na kura ya maoni, lakini bado ni matokeo yao mabaya zaidi kuwahi kutokea.

Chama cha Kitaifa cha Scotland sasa kinatabiriwa kupunguzwa hadi wabunge sita pekee.

Kiongozi wa mageuzi wa Uingereza Nigel Farage ameshinda kiti cha ubunge katika jaribio lake la nane, mjini Clacton, na kuahidi "hii ni hatua ya kwanza tu ya jambo ambalo litawashangaza nyote".

Chama cha Liberal Democrats pia kinatazamiwa kufaidika kutokana na kuporomoka kwa uungwaji mkono wa wahafidhina na wanatabiriwa kupata wabunge 56, upungufu wa wabunge 61 waliotabiriwa na kura ya maoni lakini bado ni matokeo yao bora zaidi tangu 2010.