Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefukuzwa kutoka chama cha African National Congress (ANC) ambacho aliwahi kukiongoza, baada ya kukipigia kampeni chama pinzani katika uchaguzi mkuu wa Mei 29.
Kamati ya nidhamu ya ANC ilimpata Bw Zuma na hatia ya "kukiuka maadili " ya chama kwa kujiunga na uMkhonto we Sizwe (MK), na imempa muda wa wiki tatu kukata rufaa dhidi ya uamuzi wake.
"Jukwaa lake ni hatari, linatoa wito wenye msimamo mkali katika siasa zetu ambao unaweza kuchochea machafuko ya kijamii," ANC ilisema katika taarifa.
uMkhonto we Sizwe kimesema kuwa Bw Zuma hakuarifiwa kuhusu uamuzi uliochukuliwa na " kangaroo court" [Mahakama isiyo rasmi].
Bw Zuma, 82, alikuwa kiongozi mkongwe wa ANC lakini alitofautiana na chama hicho baada ya kulazimishwa kujiuzulu kama rais mwaka wa 2018 kutokana na kashfa za ufisadi. Siku zote amekana kufanya kosa lolote.