Muhtasari
• Shirika la WHO limetangaza mlipuko wa ugonjwa wa mpox katika baadhi ya maeneo ya Afrika kuwa dharura ya afya ya umma.
Wakala wa afya ya umma nchini Sweden imerekodi kile inachosema kuwa ni kisa cha kwanza cha aina mpya ya ugonjwa wa mpox nje ya bara la Afrika.
Mtu huyo aliambukizwa alipokuwa akikaa katika eneo la Afrika ambako kwa sasa kuna mlipuko mkubwa wa mpox Clade I, shirika hilo lilisema.
Habari hizo zinakuja saa chache baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza kwamba mlipuko wa ugonjwa wa mpox katika baadhi ya maeneo ya Afrika sasa ni dharura ya afya ya umma ambayo inatia wasiwasi kimataifa.
Takribani watu 450 walikufa wakati wa mlipuko wa awali katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.