logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mahindi yenye sumu yazua hofu Zambia baada ya mbwa 400 kufa

Mbwa takriban 400 wanahofiwa kufa mwezi mmoja uliopita baada ya kula mahindi yenye sumu na huenda binadamu wakawa hatarini pia.

image
na Samuel Maina

Habari22 August 2024 - 04:02

Muhtasari


  • •Mbwa takriban 400 wanahofiwa kufa mwezi mmoja uliopita baada ya kula mahindi yenye sumu na huenda binadamu wakawa hatarini pia.

Mbwa takriban 400 wanahofiwa kufa mwezi mmoja uliopita nchini Zambia baada ya kula mahindi yenye sumu na huenda binadamu wakawa hatarini pia, waziri wa afya wa nchi hiyo amesema.

Elijah Muchima alitangaza kwamba takriban nusu ya sampuli 25 zilizochukuliwa kutoka kwa kampuni za kusaga mahindi zilipatikana kuwa na viwango vya juu sana vya aflatoxin, dutu yenye sumu inayozalishwa na kuvu.

Mahindi ni chakula kikuu nchini Zambia na Bw Muchimi alisema matokeo ya sampuli zilizochukuliwa "yanatia wasiwasi mkubwa kutokana na athari nyingi za kiafya kwa [watu]".

Shirika la Chakula Duniani (WHO) limesema kuwa kuna ushahidi kwamba sumu kuvu inaweza kusababisha saratani ya ini kwa binadamu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved