Polisi walisema washukiwa wawili pia waliuawa walipokuwa wakijaribu kushambulia vikosi vya usalama.
Takribani watu 10 wamethibitishwa kufariki,na wengine 8 wamelazwa hospitali baada ya kujeruhiwa katika shambulizi lililotekelezwa katika Wilaya ya Kigadi,Magharibi mwa Uganda,
Polisi na Jeshi la Uganda UPDF lilithibitisha jumatano.
‘’Taarifa za awali zinaonesha kwamba wanakikundi cha madhehebu ya kidini,ambacho jina lake halijafahamika walishambulia familia ambazo wengi wao ni jamaa zao kwa kuwakata kwa kifaa chenye ncha kali na kusababisha vifo na majeruhi’’alieleza Mejaj Bilal Katamba baada ya shambulizi la saa tatu usiku katika Kijiji cha Muzizi.
Kwa mujibu wa Meja Katamba Jeshi la Uganda na Polisi wameanza msako kuwabaini washukiwa wa shambulizi hilo wakati uchunguzi unaendelea.
Katika taarifa nyingine,msemaji wa polisi katika mkoa wa Albertine SP Julius Allan Hakiza aliwataja waliouawa miongoni mwao Watoto wanne.
‘’Wengine 8 wamelazwa katika vituo vya afya huko Kyaterekera.Jopo la maafisa polisi likiongozwa na DPC Kagadi Ampurira Kenneth na maafisa wa Jeshi,wanashughulikia tukio hilo.
‘’Tunachunguza tukio hili,na sababu za shambulizi hili ambazo bado hazijafahamika.Tunaisihi jamii kutoa taarifa zozote zinazohusiana na tukio hili.Ushirikiano wenu ni muhimu ili kuwafikisha wahusika mbele ya sheria’’SP Hakiza aliongeza