logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Netanyahu aikosoa ICC kwa kutoa waranti ya kukamatwa kwake

ICC pia ilitoa waranti ya kukamatwa kwa kamanda wa Hamas Mohammed Deif ambaye Israel inasema aliuawa huko Gaza mwezi Julai.

image
na BBC NEWS

Kimataifa22 November 2024 - 07:08

Muhtasari


  • Alisema ICC inawashtumu kwa kutumia ''uongo'' kwamba "tunawalenga raia kimakusudi wakati tunafanya kila tuwezalo kuepusha mauaji ya raia".


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelaani uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita na Uhalifu (ICC) wa kutoa waranti ya kukamatwa kwake akisema ni "chuki" dhidi yake na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant.

Alisema ICC inawashtumu kwa kutumia ''uongo'' kwamba "tunawalenga raia kimakusudi wakati tunafanya kila tuwezalo kuepusha mauaji ya raia".

ICC pia ilitoa waranti ya kukamatwa kwa kamanda wa Hamas Mohammed Deif ambaye Israel inasema aliuawa huko Gaza mwezi Julai.

Majaji wa ICC walisema kulikuwa na "sababu za kuridhisha" kuamini kuwa watatu hao "wana kesi ya kujibu" kwa uhalifu wa vita kati ya Israel na Hamas.

Rais wa Marekani Joe Biden aliitaja hatua ya ICC dhidi ya maafisa wa Israel kuwa "ya kuchukiza".



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved