logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu milioni 24.6 Sudan wakumbwa na njaa, mashirika ya umoja wa mataifa yasema

FAO, WFP na UNICEF yameonya kuwa baa la njaa litazidi mwakani ikiwa msaada wa dharura na wa kibinadamu hautapelekwa nchini humo

image
na Brandon Asiema

Kimataifa27 December 2024 - 15:36

Muhtasari


  • Taifa la Sudan limekumbwa na vita vya venyewe kwa wenyewe kati ya jeshi la serikali na jeshi la Rapid Support Forces RSF vilivyoanza mwka wa 2023 Aprili.
  • FAO imesema ina wasi wasi kuhusu kutanuka kwa ukosefu wa usalama wa chakula nchini Sudan ambapo watu wanazidi kutumbukia katika dharura na baa la njaa.


Takwimu mpya zilizotolewa na shirika la chakula na kilimo(FAO) la umoja wa mataifa kwa ushirikiano na mpango wa chakula duniani(WFP) na mfuko wa dharura wa watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umeashiria kuwa Zaidi ya watu milioni 24.6 nchini Sudan wanakumbwa kwa ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula nchini humo.

Mashirika hayo ya kimataifa katika ripoti yao ya kuhakiki ripoti ya awali ya baa la njaa iliyodhibitishwa miezi mine baada ya baa hilo la njaa kuripotiwa. Ripoti hiyo iliyotolewa Disemba 24, 2024, imesema kwamba maeneo mengi haswa kwenye kambi ya ZAMZAM iliyo kaskazini mwa Darfur na magharibi mwa Nuba zimetambuliwa kuwa na baa la njaa, mamilioni ya wakaazi wakikosa chakula na lishe bora.

Ripoti hiyo imeonya kwamba ikiwa msaada wa kibinadamu wa haraka na uasidizi wa kimataifa hautatolewa kwa wakati unaostahili, baa la njaa litasambaa hata zaidi katika mwaka wa 2025 na kuhatarisha maisha ya mamilioni ya watu haswa watoto kuzidisha janga hilo ambalo ni miojawapo wa majanga mabaya ya njaa kuwahi kushuhudiwa.

Aidha, imebainika kwamba migorogoro, kuhama na kukosa kufikiwa kwa misaada ya kibinadamu ndio imechangia zaidi ongezeko hilo la baa la njaa katika maeneo ya Darfur tangu kuripotiwa kwa janga hilo mnamo Agosti mwaka 2024.

Taifa la Sudan limekumbwa na vita vya venyewe kwa wenyewe kati ya jeshi la serikali na jeshi la Rapid Support Forces RSF vilivyoanza mwka wa 2023 Aprili.

Hata hivyo mashirika ya FAO, WFP na UNICEF zimeomba jamii ya kimataifa kuweka kipaombele ufadhili wa msaada wa kibinadamu na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia wa kusitisha mapigano katika vikwazo vya kuwafikia watu wanaohitaji msaada.

Mkurugenzi wa dharura na udhibiti wa FAO Rein Paulsen alisema kwamba lina wasi wasi kuhusu kutanuka kwa ukosefu wa usalama wa chakula nchini Sudan ambapo watu wanazidi kutumbukia katika dharura na baa la njaa.

“FAO ina wasiwasi  mkubwa kuhusu hali mbaya ya usalama wa chakula nchini Sudan, hasa katika kambi ya wakimbizi ya ndani Zamzam na makazi mengine katika maeneo yaliyoathiriwa na migorogoro, ambapo hali inazidi kwa mbaya na watu wengi Zaidi wanaingia katika hali ya dharura au njaa.”  Alisema Rein Paulsen.

Aidha, ripoti ya mashirika hayo imesema kwamba kuna baadhi ya maeneo kama vile Khartoum ns Al Jazeera ambayo tayari yanashuhudia baa la njaa ya kiwango cha 5. Kwenye maeneo hayo, kumekosekana data ya hivi karibuni ambayo inakuwa ni vigumu kubaini haswa jinsi hali ilivyo kwenye maeneo hayo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved