Kampuni ya anga inayounda, kutengeneza na kuhudumia ndege za kibiashara na kijeshi ya Boeng inaendelea na utengenezaji wa ndege maalum inayotumika na rais wa Marekani maarufu kama Air Force One ambayo inatarajiwa kuanza kutumika na rais mteule Donald Trump baada ya kumalizika kutengenezwa.
Mnamo Februari mwaka 2018, katika muhula wake wa kwanza uongozini, Donald Trump na kampuni ya Boeng waliafikiana kutengenezwa kwa ndege mbili za Air Force One ambazo ziligharimu dola bilioni 3.9 (sawia na shillingi bilioni 504.855). Ndege hizo zilistahili kukamilika kufikia mwaka wa 2021.
Hata hivyo kampuni hiyo inaendelea na ujenzi wa ndege hizo mbili na zinatarajiwa kukamilika mwaka ujao. Hii ni kwa mujibu wa chombo cha habari cha kimataifa cha BBC.
Kampuni ya Boeng pia imechangia dola milioni moja (Ksh 129.45) kwa ajili ya shughuli ya uapisho wa rais mteule Donald Trump utakaofanyika tarehe 20, Januari mwaka huu.
Boeng imejiunga na kampuni nyingine ikiwemo Google, Meta, Chevron, Ford, Toyota, General Motors na nyingine kutoa pesa kwa kamati ya uapisho wa rais Donald Trump kuingia ikulu ya White House.
Ndege ya Air Force One ni ya kipekee ambayo huyumiwa na marais wa Marekani. Ndege hiyo aina ya Boeng 747-200B kwa jina lingine VC-25 ina vigezo vya hali ya juu.
Ndege hiyo ina chumba cha rais, chumba cha mamkuli na chumba
cha mikutano, duka la dawa, vifaa vya matibabu ya dharura, na gali. Pia ndegeg
hiyo inaweza kuongezwa mafuta ikiwa angani wakati wa dharura.