Uamuzi wa Kesi kubwa zaidi inayomhusisha Imran Khan na mkewe imetolewa na mahakama ya
kupinga ufisadi katika gereza la mji wa Rawalpindi ambapo Khan amekuwa
akizuiliwa kutoka Agosti 2023.
Nyota huyo wa zamani wa kriketi, anaye umri wa miaka 72, alikuwa amefunguliwa mashtaka kwamba yeye na mkewe walipewa zawadi ya ardhi na mwanabiashara wa mali isiyohamishika wakati akihudumu kama waziri mkuu wa Pakistan kuanzia 2018 hadi 2022 na kutoa upendeleo haramu.
Khan na mkewe, Bushra Bibi, walikuwa wamekana mashtaka hayo huku tangazo la uamuzi huo ikicheleweshwa mara tatu.
Mkewe Imran Khan Bushra Bibi ambaye ako katika umri wa miaka 40 aliachiliwa kwa dhamana na baadaye kukamatwa tena baada ya kuhusishwa na kesi hilo, hii ni kutokana na ripoti iliyotolewa na kituo cha habari cha Geo News.
Waendesha mashtaka wanasema mfanyabiashara huyo, Malik Riaz, aliruhusiwa na Khan kulipa faini ambayo alitozwa katika kesi nyingine kutoka kwa pesa hizo hizo zilizoibiwa za pauni za Uingereza milioni 190 (dola milioni 240) ambazo zilirejeshwa Pakistan na mamlaka ya Uingereza mnamo 2022. kwa Hazina ya Taifa.
Khan amekana kufanya makosa hayo na kusisitiza kuwa hana hatia tangu kukamatwa kwake 2023 na kudai kwamba mashtaka yote dhidi yake ni njama ya wapinzani wake kujaribu kumzuia kurejea afisini.
Waziri huyo wa kitambo aidha ameachiliwa huru na hukumu zake kusitishwa kwa mara mingi isipokuwa moja ya madai ya kuwachochea wafuasi wake kuvamia vituo vya kijeshi ili kupinga kukamatwa kwake Mei 9, 2023.
Wafuasi wa Khan wameongoza msururu wa maandamano tangia tukio hilo la May 9 lilichangia kukamatwa kwa Imran Khan.
Khan ambaye aligatuliwa serikalini kupitia kura ya kutokuwa na Imani bungeni 2022, hapo awali alipatikana na hatia kwa tuhuma za rushwa, kufichua siri rasmi ya kiserekali, kukiuka sharia za ndoa katika hukumu tatu tofauti na kuhukumiwa miaka 10, 14 na saba mtawalia
Chini ya sheria za Pakistan atatumikia masharti kwa wakati mmoja hii ni kumanisha kuwa atakuwa anahudumia kifungo kirefu zaidi za hukumu.
Baada ya kutangazwa kwa uamuzi huo na mahakama wanasheria kutoka katika upande wa Imran Khan walifika nje la jengo la bunge katika jiji kuu, Isamabad wakisema kuwa waziri huyo mkuu wa kitambo amehukumiwa kimakosa.