TikTok ilianza kurejesha huduma zake nchini Marekani siku ya Jumapili baada ya masaa kadhaa ya marufuku.
Hii ilikuwa baada ya Rais mteule Donald Trump kusema atatoa agizo kuu la kuipa programu hiyo ahueni atakapoingia madarakani Jumatatu.
"Kusema ukweli, hatuna chaguo. Tunapaswa kuokoa mtandao," Trump alisema katika mkutano wa Jumapili.
Trump aliongeza kuwa Marekani itatafuta ubia wa kurejesha programu hiyo ya kushiriki video fupi inayotumiwa na Wamarekani milioni 170.
Kabla
ya uthibitisho wa Trump wa kurejea kwa TikTok, jukwaa hilo maarufu la mtandao
wa kijamii lilikuwa tayari limetuma arifa kwa watumiaji wake kuwaambia kuwa
limerudi.
TikTok pia ilitoa taarifa ya awali baada ya jukwaa maarufu la mitandao ya kijamii kuanza kurudi mtandaoni kwa baadhi ya watumiaji na huduma chache za msingi.
"Kwa makubaliano na watoa huduma wetu, TikTok iko katika mchakato wa kurejesha huduma. Asante Rais Trump kwa kutoa ufafanuzi unaohitajika na hakikisho kwa watoa huduma wetu kwamba hawatakabiliwa na adhabu (kwa) kutoa TikTok kwa Wamarekani zaidi ya milioni 170 na kuruhusu. zaidi ya biashara ndogo ndogo milioni 7 kustawi,” TikTok ilisema.
Kufikia siku ya Jumapili jioni, programu hiyo hata hivyo iliendelea kutopatikana kwa kupakuliwa kwenye maduka ya programu ya Marekani.
TikTok iliacha kufanya kazi kwa watumiaji wa Marekani Jumamosi jioni kabla ya sheria ya kuifunga kwa misingi ya usalama wa kitaifa kuanza kutumika Jumapili.
Maafisa wa Marekani walikuwa wameonya kwamba chini ya kampuni ya Kichina ya ByteDance, kulikuwa na hatari ya data ya Wamarekani kutumiwa vibaya.
Trump alisema "ataongeza muda kabla ya makatazo ya sheria kuanza kutekelezwa, ili tufanye makubaliano ya kulinda usalama wa taifa letu."
"Ningependa Marekani iwe na nafasi ya umiliki wa 50% katika ubia," aliandika kwenye mtandao wa Truth.
Trump alisema agizo la mtendaji litabainisha kuwa hakutakuwa na dhima kwa kampuni yoyote ambayo ilisaidia kuzuia TikTok kutoka gizani kabla ya agizo lake.