logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Papa Francis augua numonia Katika mapafu yake yote: Vatican imesema

Hali ya Papa bado ni ngumu kulingana na ripoti kutoka Vatican.

image
na Japheth Nyongesa

Kimataifa19 February 2025 - 10:38

Muhtasari


  • Licha ya hayo, Vatican imesema kuwa, Papa huyo amebaki katika "roho nzuri" na ametumia siku yake "kusoma, kupumzika na kusali".
  • Papa Francis pia ametoa shukrani zake kwa watu wanaomutakia wema na kuwataka wamuombee.

iongozi wa makanisa ya kirumi katholiki Papa Francis amethibitishwa kuugua homa ya mapafu [Pneumonia ] na hali yake bado ni ngumu kulingana na ripoti kutoka Vatican.

Papa huyo mwenye umri wa miaka 88 amekuwa akisumbuliwa na maambukizi ya mfumo wa kupumua kwa zaidi ya wiki moja na alilazwa katika hospitali ya Gemelli mjini Rome siku ya Ijumaa.

"Uchunguzi wa kifua kufuatilia CT Scan ambayo Baba Mtakatifu alifanyiwa jana jumanne ilionyesha mwanzo wa homa ya mapafu,  ambayo inahitaji tiba ziada ya dawa," Vatican ilisema.

Licha ya hayo, Vatican imesema kuwa, Papa huyo amebaki katika "roho nzuri" na ametumia siku yake "kusoma, kupumzika na kusali".

Papa Francis pia ametoa shukrani zake kwa watu wanaomutakia wema na kuwataka wamuombee.

Kabla ya kuingia kwake hospitalini wiki iliyopita, Papa alikuwa na dalili za ugonjwa wa bronchitis kwa siku kadhaa na alikuwa akiwapa maafisa wengine kusoma hotuba zilizotayarishwa katika hafla.

Alikuwa amepangiwa kuongoza matukio kadhaa mwishoni mwa wiki kwa ajili ya Mwaka Mtakatifu wa Kikatoliki wa 2025 ambao unamalizika Januari ya mwaka ujao, hata hivyo matukio yote ya umma kwenye kalenda ya Papa yalifutiliwa mbali hiyo Jumapili.

Siku ya Jumatatu, Vatican ilisema madaktari walikuwa  wamebadilisha tiba ya dawa ya Papa kwa mara ya pili baada ya kuingia hospitalini ili kukabiliana na kile kilichodhaniwa kuwa "maambukizi ya njia ya kupumua".

Papa ambaye ameathirika zaidi na maambukizi ya mapafu kutokana na kuwa na ugonjwa wa kupooza kama mtu mzima na lingine ni kwamba sehemu ya mapafu yake yaliyoondolewa akiwa na umri wa miaka 21.

Wakati wa miaka yake 12 kama kiongozi wa kanisa Katoliki la Kirumi, Muargentina huyo amelazwa hospitalini mara kadhaa ikiwa ni pamoja na Machi 2023 wakati alikaa hospitalini kwa siku tatu mfululizo kutokana na bronchitis.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved