

Kikosi cha kivita kisichotumia rubani cha angani kilihudhuria gwaride la kijeshi mjini Beijing, mji mkuu wa China, Septemba 3, 2025. China Jumatano iliandaa mkusanyiko mkubwa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Upinzani dhidi ya Uvamizi wa Kijapani na Vita vya Ulimwengu dhidi ya Ufashisti. (Xinhua/Xing Guangli)
China iliandaa gwaride kubwa la kijeshi katikati ya Beijing Jumatano kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi wake katika Vita vya Pili vya Dunia, na kusisitiza dhamira ya nchi hiyo ya maendeleo ya amani katika dunia ambayo bado imejaa misukosuko na hali za kutokuwa na uhakika.


Kikosi cha walinda amani wa China chini ya Umoja wa Mataifa kilihudhuria gwaride hilo. (Xinhua/Jiang Kehong)
Kikosi cha mashambulizi ya ardhini kilishiriki katika gwaride hilo. (Xinhua/Jiang)
Kikosi cha ulinzi wa anga kutoka meli kilipita katika Uwanja wa Tian’anmen wakati wa gwaride la kijeshi. (Xinhua/Yao Dawei)
Kikosi cha makombora ya kupambana na meli kilihudhuria gwaride. (Xinhua/Li He)
Vikosi vya silaha vizito vilishiriki katika gwaride hilo. (Xinhua/Wang Peng)
Kikosi cha makombora ya mwendo wa kasi wa sauti kilihudhuria gwaride. (Xinhua/Zhang Tao)
Kikosi cha ndege za mafuta na ndege zinazopokea mafuta hewani kilishiriki katika gwaride hilo. (Xinhua/Sun Fanyue)
Picha hii iliyopigwa Septemba 3, 2025 inaonesha kikosi cha ndege za kivita. (Xinhua/Bai Xueqi)