logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume afungwa miaka 52 jela kwa kumuua na kumtoa kafara mtoto wa miaka 5

Tukio hilo lilitokea mwaka 2017.

image
na Davis Ojiambo

Habari03 November 2023 - 06:44

Muhtasari


  • • Kufuatia uamuzi huo, mawakili wa haki za mtoto waliohudhuria mahakamani waliipongeza mahakama kwa uamuzi huo.

Mahakama kuu ya Uganda imemhukumu mtu mmoja kifungo cha miaka 52 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtoto wa miaka mitano na kumtoa kafara, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Hakimu David Batema alimhukumu Hassan Kafudde kifungo cha miaka 52 jela pamoja na Issa Muyita, baba wa marehemu aliyehukumiwa miaka 25 kwa kumuua Juma Muyita, 5 ambaye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Mirembe Junior iliyoko Kawempe mwaka 2017.

Katika uamuzi wake, Jaji Batema alibainisha kuwa adhabu hiyo inapaswa kuwa kizuizi kwa wahalifu wengine.

Kufuatia uamuzi huo, mawakili wa haki za mtoto waliohudhuria mahakamani waliipongeza mahakama kwa uamuzi huo.

Akihutubia wanahabari, msemaji wa DPP Jackline Okui alikaribisha hukumu hiyo ambayo alisema itasaidia kutenda haki.

Pia alitoa wito kwa wazazi kujiepusha na tabia ya kuwatoa watoto wao wenyewe ili kujipatia mali, akibainisha kuwa tabia hiyo imekithiri katika kitongoji cha Busoga.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved