Kevin Kangethe anyimwa dhamana na mahakama nchini Marekani

Alifikishwa mbele ya Mahakama ya Juu ya Suffolk iliyoko Pemberton Square, Boston, Septemba 3, 2024 na kukana kumuua Margaret Mbitu.

Muhtasari

• Zaidi ya hayo, mahakama ilisikia kuwa mshukiwa na marehemu walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi ambao ulikuwa umekumbwa na ripoti za unyanyasaji wa kinyumbani.

KEVIN KANG'ETHE AKIWASILI MAREKANI.
KEVIN KANG'ETHE AKIWASILI MAREKANI.
Image: ODPP//X

Mshukiwa wa mauaji ya mpenzi wake nchini Marekani, Mkenya Kevin Kang’ethe amenyimwa dhamana na mahakama inayoshugulikia kesi yake nchini Marekani.

Ofisi ya mkuu wa mashtaka ya umma nchini Kenya kupitia ukurasa wa X walitaarufu kwamba Kang’ethe kwa sasa anashikiliwa korokoroni nchini Marekani baada ya kukana mashtaka ya mauji.

Kang’ethe alisafirishwa kutoka Kenya kwenda Marekani siku chache zilizopita baada ya kutoroka Marekani ambapo alituhumiwa kumuua mpenzi wake katika uwanja wa ndege mwaka jana.

“Kevin Kangethe alinyimwa dhamana/bondi na mahakama ya Marekani (Marekani) baada ya kukana shitaka la mauaji. Kangethe alirejeshwa Marekani kutoka Nairobi mnamo Septemba 1, 2024, baada ya mchakato uliofaulu wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson M. Ingonga, OGW.”

“Alifikishwa mbele ya Mahakama ya Juu ya Suffolk iliyoko Pemberton Square, Boston, Septemba 3, 2024 na kukana kumuua Margaret Mbitu. Mahakama iliamua kuwa atazuiliwa bila dhamana, bila upendeleo. Upande wa mashtaka unaongozwa na ADA Mark Lee,” ODPP aliarifu kupitia X.

Zaidi ya hayo, mahakama ilisikia kuwa mshukiwa na marehemu walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi ambao ulikuwa umekumbwa na ripoti za unyanyasaji wa kinyumbani.

 

Kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya tarehe ya awali ya kusikilizwa mbele ya sehemu ya Mauaji mnamo tarehe 5 Novemba 2024 saa mbili usiku.