Mwanamume wa umri wa miaka 52 amefungwa jela miaka minne na
nusu kwa makosa ya kumhada mkewe kuelekea nchini Sudan kisha kumwacha nchini humo
akihangaika.
Mahakama moja nchini Australia imetoa hukumu hiyo baada ya
kubaini kuwa mwanamume huyo alimlaghai mkewe kusafiri kuelekea Sudan kabla ya
kuchukua watoto wake wawili pamoja na hati ya kusafiri ya mkewe na kurudi Australia.
Jaji aliyesikiliza kesi hiyo Frank Gucciardo, alisema kwamba
makosa aliyoyatekeleza jamaa huyo yalihusisha mipango ya makusudi kwani hakumtaarifu
mkewe kuwa alikuwa ameondoa visa yake(mkewe) mnamo mwaka wa 2014 jambo ambalo
ikiwa mkewe angejaribu kuomba ombi ya kurejeshewa, ombi hilo lingekataliwa.
Jaji Frank alisema kwamba kitendo alichomfanyia mkewe
kilikosa uungwana akiongeza kuwa mwanamke huyo alikuwa na huzuni mno wa kuondokewa
kwa watoto wake.
Mkewe mshukiwa aliishi nchini Sudan kwa takribani mwaka
mmoja na miezi minne, kabla ya kupata usaidizi wa kisheria na uhamiaji kutoka
kwa ubalozi wa Australia ulioko nchini Misri.
Mwanamke huyo ambaye jina lake lilibanwa kwa sababu za
kuisalama, alipata visa kutoka kwa wizara ya mambo ya ndani iliyomruhusu
kusafiri hadi Australia mwishoni mwa mwezi Februari mwaka wa 2016.
Hata hivyo mwanamume huyo alikana shtaka dhidi yake la
kumdanganya mkewe.
Aidha, wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo kabla ya kutolewa
kwa hukumu, mahakama hiyo ilielezwa na mke wa mwanamume huyo kwamba alikuwa na
uzoefu mbaya sana kwani aliwahi kwama na watoto wake.
Katika barua iliyosomwa kortini, mkewe ambaye
waliwachana alisema
kuwa watoto wake walikuwa wamevumilia "mateso yasiyofikirika" baada
ya kuondolewa bila idhini yake. Alisema kuwa mmoja wa watoto wake anakabiliwa
na wasiwasi mkubwa wa kutengana na hadi sasa huwa anahofia mama yake hatarudi anapoondoka.