Mahakama ya Vihiga imemhukumu kifungo cha maisha jela, jamaa mmoja aliyepatikana na hatia ya kumnajisi msichana wa umri wa miaka 10.
Katika hukumu ya korti hiyo, ilibainika kuwa upande wa mashtaka ukiongozwa na Mary Bosibori uliwasilisha ushahiodi wa kutosha dhidi ya mshtakiwa. Mahakama ilisema kuwa ushahidi uliowasilishwa kutoka kwa mashahidi watano kwenye kesi hiyo pamoja na vidhibitidho na ushuhuda ulipita kiwango cha kutiliwa shaka.
Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma ODPP, ilisema kuwa korti ilipata ushahidi uliotolewa mahakamani ulionyesha taswira kamili isiyoweza kukanushwa ya tukio lililofanywa na mshtakiwa.
“Upande wa mashtaka ukiongozwa na Mary Bosibori ulithibitisha kesi bila shaka kupitia vielelezo na ushuhuda kutoka kwa mashahidi watano. Ushahidi huu, mahakama ilisema kwamba ulitoa taswira kamili na isiyoweza kukanushwa ya uhalifu uliofanywa na mshtakiwa.” ODPP ilisema kwenye ukurasa wake wa X.
Mahakama hiyo aidha ilimpata mshtakiwa na hatia kinyume na kifungu
cha 8 ibara ya 1 kilichosomwa kwa pamoja na kifungu cha 8 ibara ya 2 cha sheria ya vitendo vya ukatili wa kijinsia
nambari 3 ya mwaka 2006.