Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 22, kutoka Sengerema mkoani Mwanza nchini Tanzania amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kupatikana na makosa ya kuvalia sare za jeshi.
Mahakama ya wilaya ya Sengerema ilimkuta na hatia jamaa huyo kwani ni kinyume cha sheria kwa raia wa kawaida kuvalia sare za jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) bila ruhusa.
Wakati wa kusikiliza mashtaka dhidi yake, mshukiwa alikiri hatia dhidi yake huku akimwomba hakimu kumwachilia huru kwa kosa hilo.
Mshukiwa alimweleza hakimu kuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kupatikana na makosa wakati hakimu alimtaka kueleza ni kwa nini asihukimiwe adhabu ya kuhudumu kifungo katika gereza.
“Naomba nisamehewe kwa sababu ni kosa la kwanza. Nilivaa kwenda kumwonyesha mchumba wangu kuwa mimi ni askari ili asinikatae.” Alisema mshukiwa wakati wa kujitetea mbele ya hakimu.
Hata hivyo, mahakama ilibaini kuwa makosa ya jamaa huyo ilikuwa kinyume cha sheria kifungu cha 178(1) cha sheria cha kanuni ya adhabu sura ya 16 ya mwaka 2022.
Aidha, mshukiwa huyo alikiri kuwa alivalia sare hizo ili
kumfurahisha mpenzi ndio amkubali.
Mshukiwa alikamatwa mnamo Disemba 5 mwaka jana
katika kijiji cha Kasisa