Mshukiwa wa wizi raia wa Uganda imeratibiwa kusikilizwa mwezi Machi katika mahakama ya Makadara.
Kesi hiyo inayomhusisha mwanamke aliyekuwa mfanyakazi wa nyumbani kwa Mkenya mmoja katika eneo la Eastleigh ilitajwa katika mahakama ya Makadara ambapo mahakama hiyo ilimnyima mshukiwa dhamana ya kuachiliwa kabla ya kesi hiyo kusikilizwa.
Mwanamke huyo maarufu kama Eva, anakabiliwa na mashataka ya wizi wa mali kutoka kwa mwajiri mwake mnamo Novemba mwaka 2024 akiwa amejihami kwa silaha butu.
Upande wa mashtaka katika kesi iliyowasilisha mbele ya mahakama ya Makadara ilisema kwamba mshukiwa huyo alikuwa amejihami kwa nyundo kama silaha ya mashambulizi wakati akitekeleza wizi huo.
Eva, anadaiwa kuiba simu yenye thamani ya shilingi elfu thelatini kutokakwa mwajiri wake pamoja na kipatakilishi chenye thamani ya shilingi laki moja na elfu kumi. Vile vile mshikuwa anadaiwa kuiba dhahabu yenye uzani wa gramu 22 inayokadiriwa kuwa yenye thamani ya shilingi laki mbili na elfu kumi.
Mwanamke huyo raia wa Uganda alikamatwa jijini Nairobi katika stendi ya mabasi eneo la Kariakor akisubiri kuabiri basi la kuelekea nchini Uganda.
Eva alishtakiwa pamoja na mshukiwa wa pili ambaye hakuwa mahakamani wakati wa kusomewa mashataka.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi dhidi yake na mshukiwa wa
pili, mahakama ya Makadara ilidinda kumwachilia kwa dhamana baada ya upande wa
mashtaka kupinga ombi ya mshukiwa kuachiliwa upande wa mashtaka ukidai kwamba
si Mkenya na anaweza kutoroka nchini ilikukwepa kujiwasilisha nchini wakati wa kusikilizwa
kwa kesi dhidi yake.