Ni kesi ya pili kuwasilishwa mahakamani ikitaka majaji wote wa mahakama ya upeo waondolewe, itakumbukwa kuwa kesi sawia na hii ilikuwa imewasilishwa na aliyekuwa rais wa mawakili Nelson Havi mnamo Januari 13,2025 kwa tume ya huduma za majaji(JSC).
Bwana Havi anawakashifu majaji wa mahakama ya upeo kwa madai ya kukosa maadili.
Shinikizo hizi zimeongezeka baada ya mawakili wengine 13 kuwasilisha kesi nyingine mpya wakitaka majaji wote wa mahakama ya juu wang'atuliwe ofisini huku kukiwa na vitisho vya mawakili wote kugoma jambo ambalo mahakama imeowaonya wasichukue mkondo huo kusambaratisha shughuli za mahakamani.
Siku ya Jumanne, mawakili wanaofanya kazi kwa afisi ya wakili Ahmednasir Abdulillah(LLP)waliwasilisha kesi kortini kwa tume ya huduma za majaji wakimushutumu Jaji mkuu Martha Koome pamoja na majaji wengine wa mahakama ya upeo kwa kutoa uamuzi unaowazuia kuonekana katika mahakama ya upeo kwa vyovyote vile.
Uamuzi wa kumzuia wakili Ahmednasir pamoja na mawakili wanaofanya kazi chini ya huduma yake ya mawakili iliyotolewa Januari 2024 kutokana na kushambulia majaji wa mahakama mitandaoni, jambo ambalo liliwaathiri hata mawakili wanaofanya kazi chini ya huduma yake ya sheria.
Hayo yakiendelea, muungano wa mawakili unazidi kutoa shinikizo za kugoma kutokana na amri hiyo ya kumzuia wakili Ahmed Nasir pamoja na mawakili walio chini yake, ni vita ambavyo vimeendelea kwa muda huku mahakama ikiwaonya kuhusu mpango wao wa kutaka kugoma ambao bila shaka anaazimia kusambaratisha huduma na shughuli zote za mawakili mahakamani.
Msemaji wa mahakama Paul Ndemo katika taarifa yake alisema kuwa kuna kesi nne ambazo ziko katika mahakama kuu,mahakama ya rufaa na mahakama ya afrika mashariki kuhusu jambo hilo hilo kwa hivyo kutishia kugoma kutatoa picha mbaya na kushusha hadhi za mahakama jambo ambalo linaweza vutia adhabu kisheria.
Mawakili hao walisema kuwa mnamo Januari 18 kuna barua ambayo Ahmednasir Abdulillah aliandikiwa na mawakili walio chini ya huduma yake ya sheria hawakufafanuliwa mustakabali wao katika suala hilo jambo ambalo limeibua hali ya sintofahamu kati ya majaji wa mahakama ya upeo na muungano wa mawakili nchini wakitaka kuhakikisha kuwa wanashinikiza matakwa yao yasikilizwe na hata kuandamana na kulemaza huduma zote za kisheria pamoja na kutwaa sehemu maalumu za huduma za sheria hadi kilio chao kisikilizwe .
Itakumbukwa kuwa kesi sawia na hii ilikuwa imewasilishwa na aliyekuwa rais wa mawakili Nelson Havi akiwashutumu majaji hao kwa ukosefu wa maadili.