Afueni kwa Majaji wa mahakama ya upeo mahakama ya Narok ikisitisha kwa muda kesi ya JSC
Mahakama kuu ya Narok
ilitoa uamuzi wa muda kuzuia tume ya Huduma kwa mahakama JSC kutaka
majibu ya mashitaka yaliokuwa yamewasilisha
kortini dhidi ya majaji wa mahakama ya upeo.
Uamuzi huo unatoa afueni ya muda kwa Jaji mkuu Martha Koome,Naibu jaji mkuu
Philomena Mwilu,Jaji Mohammed Ibrahim,Jaji Smokin Wanjala,Jaji Njoki Ndung’u
,Jaji Isaac Lenaola na Jaji William Ouko waliokuwa wakikabiliwa na vita vya
kisheria kuhusu uwajibikaji na uhuru wao kikazi kama majaji.
Jaji Charles Kariuki alipokuwa akitoa uamuzi wa kesi hiyo alitaja
kesi hiyo kama ya dharura na kutoa uamuzi wa kusitisha kwa muda mchakato wa kutaka
majibu kwa wahusika waliotajwa kesini.
Akitoa uamuzi huo Jaji alieleza kuwa shinikizo la JSC kutaka
majibu ya kesi yao iliyowasilishwa dhidi
ya majaji saba wa mahakama ya upeo ilikosa utaratibu maalum wa kuiendesha.
Tume ya kuangazia utendakazi wa Majaji JSC ilikuwa
imewasilisha kesi kortini mnamo Januari 27,2025 ikitaka majaji kujibu
mashitaka ya kesi nambari 35 ya 2024,72
ya 2024 na 3 ya 2025 mtawalia.
Mahakama hiyo ilitoa mwongzo kwa tume hiyo ya JSC ikitaka
maelezo ya muongozo wa kisheria ambao JSC iliokuwa nao na iliokusudia kuutumia
kuwaadhibu na kuwaadhibisha Majaji.
Hata hivyo Korti
ilisimamamisha mchakato huo wa JSC kutaka kuendelelea na Kesi hiyo hadi matakwa
yote yatimie.
Hata hivyo mahakama ilitoa maelezo ikisema kuwa washitaki ni
lazima wawasilishe majibu yao chini ya siku 21 baada ya uamuzi huo kutolewa na
kila pande zote husika zipewe nyaraka husika ndani ya siku 14.
Kesi hiyo imeratibiwa kusikilizwa mnamo machi 12,2025 ili kudhibitisha iwapo maamuzi ya muongozo uliotolewa ka korti ulifutwa ipasavyo,gharama ya kusikilizwa kwa kesi hiyo itatolewa wakati wa mwisho wa kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Itakumbukwa vyema kuwa siku chache zilizopita kulikuwa na
shinikizo za mawakili wakishutumu uamuzi wa mahakama kuu uliotolewa wa kumzuia
wakili Ahmednasir Abdullahi na kampuni yake dhidi ya kuendesha shughuli zozote
za kisheria mahakani miongoni mwa madai mengini.