
Waititu alikuwa amewasilisha kesi mahakamani akitaka mahakama kuu kumpa idhini ya kuachiliwa kwa dhamana jambo ambalo mahakama ya chini ilikuwa imepinga wakati wa kuamuliwa kwa kesi yake.
Jaji wa Mahakama Kuu Lucy Njuguna aliamua kwamba Waititu anatalazimika kukaa kizuizini hadi Aprili 23 wakati mahakama itatoa uamuzi ikiwa inaweza kubadilisha rufaa yake.
Gavana huyo wa zamani Jumanne, Machi 18, aliwasilisha ombi jipya la kutaka kuachiliwa kwa dhamana huku akiendelea kutumikia kifungo jela baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi.
Ombi hilo jipya lilikuja baada ya rufaa dhidi ya hukumu yake ya jela iliyowasilishwa na wakili wake ambayo bado inasubiri.
Waititu alitaka mahakama kumuachilia kwa dhamana wakati akingoja rufaa yake ambayo aliwasilisha isikilizwe na kuamuliwa. Gavana huyo wa zamani alifika mahakamani hii leo Jumatano 26 Machi kusikiliza hatima ya kesi yake ya kuachiliwa kwa dhamana.
Waititu alizungukwa na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na kiongozi wa Democratic Action Party-Kenya Eugene Wamalwa baada ya wao kufika mahakamani ili kukutana na yeye kama njia ya kuonyesha kumuunga mkono.
Mwanasiasa huyo alikata rufaa yake ya kwanza akiomba dhamana, ila mahakama ilikataa kumpa dhamana baada ya ombi lililofaulu la Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) kupinga ombi lake la kuachiliwa kwa dhamana.
Katika rufaa yake, Waititu alikuwa amesema afya yake ilikuwa mbaya, akilalamika kwa maumivu ya kifua na shinikizo la damu lakini yote haya yalionekana kuwa yasiyo na umuhimu.
Duru zinaarifu kwamba mwanasiasa huyo maafufu aliondolewa katika jela ya viwandani [industral area prison] na kuhamishiwa jela ya kamiti.