MWANAMKE mwenye umri wa miaka 39 amesimulia mahakamani kwa majonzi jinsi aligundua mumewe amekuwa akifanya mapenzi na binti yao mwenye umri wa miaka 19.
Kwa mujibu wa mwanamke huyo aliyetoa ushahidi wake mbele ya
hakimu, Alifunguka kwamba mumewe mwenye umri wa miaka 45 amekuwa akifanya
mapenzi kisiri na binti yao mwenye miaka 19 katika kitanda chao cha ndoa.
Baada ya kuwafumania na kumkabili binti yake, alimwambia
kwamba babake alimwambia anafanya naye mapenzi kama ishara ya upendo kwake kama
mwanawe wa kumzaa.
Katika kesi hiyo iliyogonga vichwa vya habari jiji kuu la
Zambia, Lusaka, BM, mwenye umri wa miaka 45 alikana mashtaka mawili ya kujamiiana na
mashitaka mawili ya shambulio la aibu kwa wanawake kinyume na sheria za Zambia,
jarida moja liliripoti.
Mshitakiwa huyo alifikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi Amy
Masoja ambaye alimsomea mashitaka yote ambapo alikana kuyatenda.
Alipoitwa kwenye kizimbani cha shahidi kutoa ushahidi wake,
BB, mke kwa mshtakiwa kwa zaidi ya miaka 23 na mama kwa mwathiriwa, alitoa
ushahidi jinsi alivyogundua kuwa bintiye alikuwa akinyanyaswa na babake mzazi.
“Binti yangu MM alinieleza kuwa kati ya 2023 na 2024 kuna kitu
kilimtokea, akaniambia baba yake anafanya kitu, nikamuuliza alikuwa anamfanya
nini, akasema baba alikuwa akimshika matiti, nikamuuliza ni matiti tu ndiyo
anaguswa akanyamaza.”
"Nilimwomba amalize kusema alichoanza jana usiku. Aliniambia kuwa
siku nilipoenda kwenye Praise Overnight kwa Ushers na viongozi mwaka 2024,
alisema alibaki na baba alifanya naye mapenzi," msichana huyo
alisema.
BB alisema kitendo hicho kilitokea ndani ya nyumba, katika
chumba kikuu cha kulala, chumba cha kulala cha wanandoa.
Mama wa manusura alisema binti huyo alipomkabili baba yake
kwamba alichokuwa akifanya naye ni kibaya, mwanamume huyo alimwambia kuwa
alikuwa akifanya naye mapenzi kwa sababu anampenda.