AYUB SAVULA: Vunjeni Oka, vinara wajiunge na Raila au Ruto

Muhtasari

• Hakuna kitu kama One Kenya Alliance. Muungano huo hauendi popote katika uchaguzi mkuu wa Agosti.

• OKA haiwezi kusonga. Muungano huo ulikuwa na mkutano wa hadhara mjini Kakamega mwezi Oktoba, wa pili Naivasha mwezi Novemba na wa tatu mjini Thika mwezi Desemba.

• Njia pekee ya kutoka kwenye kinamasi hiki ni kujiunga na moja ya kambi hizo mbili (Raila na Ruto).

Mbunge wa Lugari Ayub Savula
Mbunge wa Lugari Ayub Savula
Image: MAKTABA

Hakuna kitu kama One Kenya Alliance. Muungano huo hauendi popote katika uchaguzi mkuu wa Agosti.

Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka tayari ametangaza kwamba anakabiliwa na shinikizo kuania kivyake. Mwenzake wa Kanu, Gideon Moi, hivi karibuni atahamia Azimio la Umoja linaloongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.

Sasa nani atabaki kwenye muungano changa?

Ikiwa Kalonzo atahama, kumbuka jina la Oka limehifadhiwa na watu wake, kwa hivyo historia itajirudia jinsi Kalonzo alivyoondoka na chama cha ODM Kenya.

Jambo bora la kufanya ni kwa machifu wa Oka kuvunja vazi hilo na kuungana na Naibu Rais William Ruto au kinara wa ODM Raila Odinga.

Kwa hali ilivyo, sio siri hakuna umoja katika Muungano wa One Kenya Alliance. Vinara hawatafikia lengo lao.

Raila atashinda katika duru ya kwanza, hakutakuwa na marudio. Uliona mapokezi katika uwanja wa Thika. Wakikuyu watampigia kura Tinga.

Watampa asilimia 50. Anakwenda kuwa rais.

OKA haiwezi kusonga. Muungano huo ulikuwa na mkutano wa hadhara mjini Kakamega mwezi Oktoba, wa pili Naivasha mwezi Novemba na wa tatu mjini Thika mwezi Desemba.

Sasa wamerudi tena kwa majadiliano, kupoteza wakati.

Ni wiki 28 kabla ya uchaguzi. Tuna kaunti 47. Utashughulikiaje kaunti. Ni mzaha kabisa.

Tuna maeneo bunge 290, unayashughulikia vipi ndani ya wiki 28?

Vinara wa Oka hawana mikakati ya pamoja. Muda umeyoyoma kwa hivyo wanapaswa kuvunjilia mbali muungano huo na kujiunga na mrengo wa Ruto au Raila. Kisha mchezo uanze.

Viongozi wenye misimamo mikali walisambaratisha Oka. Nilikuwa mkali kwa kumtetea Mudavadi na Kalonzo alikuwa na wake pia.

Hakuna aliyekuwa tayari kuachia mwingine. Kati ya Kalonzo na Musalia, tuliishia kwenye fujo hii.

Njia pekee ya kutoka kwenye kinamasi hiki ni kujiunga na moja ya kambi hizo mbili (Raila na Ruto).

Naungana na Raila.

Musalia akitaka kwenda kwa debe namtakia kila la kheri ila farasi ni mbili.

Mbunge huyo wa Lugari alizungumza na gazeti la Star.

IMETAFSIRIWA NA KUHARIRIWA NA DAVIS OJIAMBO.