Diverticular: Fahamu maradhi hatari ya utumbo yaliomlazimu Papa Francis kufanyiwa upasuaji

Mwaka 2014, alilazimika kukatiza hafla nyingi kutokana na tatizo la tumbo ,

Muhtasari

•Ugonjwa wa kufura kwa utumbo ni maradhi ya mfumo wa kusaga chakula tumboni ambao unahusishwa na kufura kwa vifuko ambavyo husababishwa na kuzeeka katika kuta za utumbo mdogo kulingana na Shirika la huduma za afya ya umma nchini Uingereza NHS katika ukurasa wake.

•Maradhi haya huanza kuwaathiri wagonjwa kuanzia umri wa miaka 60 na wengi ya wazee walio na umri wa miaka 80 na zaidi , kulingana na shirika la huduma ya afya ya umma nchini Uingereza NHS.

Pope Francis
Pope Francis
Image: Hisani

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis alifanyiwa upasuaji siku ya Jumapili katika hospitali ya Gemeli mjini Rome ili kurekebisha tatizo katika utumbo wake .

Kulingana na taarifa ya kanisa la Vatican, kiongozi huyo wa dini mwenye umri wa miaka 84 alifanyiwa upasuaji uliofaulu.

''Papa Francis anaendelea kujiuguza vyema kufuatia upasuaiji huo uliofanywa baada ya kudungwa sindano ya kulala'' , alisema msemaji wa Vatican Matteo Bruni.

Ugonjwa wa kufura kwa utumbo ni maradhi ya mfumo wa kusaga chakula tumboni ambao unahusishwa na kufura kwa vifuko ambavyo husababishwa na kuzeeka katika kuta za utumbo mdogo kulingana na Shirika la huduma za afya ya umma nchini Uingereza NHS katika ukurasa wake.

Watu wengi walio na maradhi hayo ya Diverticula hawana dalili na wanaweza kugundua ugonjwa huo wanapofanyiwa uchunguzi kupitia skani kwa sababu nyengine.

Hali hiyo isio na dalili huitwa Diverticulosis.

Iwapo diverticula ina dalili , kama maumivu tumboni , huitwa maradhi ya diverticular.

Lakini kunapokuwa na uvimbe ama maambukizi, na kusababisha maumivu zaidi maradhi hayo huitwa Diverticulitis.

Stenosis ni hatua ya utumbo kuwa mwembamba hatua ambayo huenda ikasababisha diverticulitis.

Dalili zinazojulikana sana ni maumivu makali katika eneo la kushoto la tumbo, ambayo huongezeka wakati mtu anapokula lakini hupungua kwa kutoa hewa chafu mwilini au kwenda haja kubwa.

Haja ngumu au kuharisha ni baadhi ya dalili nyengine pia. Hatahivyo sio kawaida kupata damu katika kinyesi.

Hatari za ugonjwa huu.

Fahamu ugonjwa wa Diverticular
Fahamu ugonjwa wa Diverticular
Image: HISANI

Haijulikani ni kwanini watu huugua ugonjwa huu lakini unaonekana kuhusishwa na umri , chakula , maisha mtu anayoishi na jeni.

Umri ni miongoni mwa sababu hatari zinazosababisha maradhi ya diverticular.

Watu wachache walio chini ya umri wa miaka 40 huugua maradhi haya.

Maradhi haya huanza kuwaathiri wagonjwa kuanzia umri wa miaka 60 na wengi ya wazee walio na umri wa miaka 80 na zaidi , kulingana na shirika la huduma ya afya ya umma nchini Uingereza NHS.

Hii ni kwasababu kuta za utumbo mkubwa hudhoofika kutokana na umri hususan katika Sigmoid - eneo la chini la tumbo.

Shinikizo la kupitisha haja kubwa - linaweza kusababisha diverticula.

Ukosefu wa chakula chenye nyuzi pia uhusishwa na maradhi haya.

Sababu nyengine zinazosababisha hatari ni pamoja na mtu kuongeza uzani, kuvuta sigara, kuwa na historia ya haja ngumu na matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maimuvi kama vile Aspirin.

Hali ya Kiafya ya Papa Francis ikoje?

Hii ndio mara ya kwanza Papa Francis kulazwa hospitalini tangu uteuzi wake 2013.

Jumapili iliopita Papa francis alikuwa katika hali yake ya kawaida wakati akitoa baraka zake za kila wiki katika kanisa la mtakatifu Peter na kutangaza kwamba alikuwa na ziara ya kuelekea Slovakia na Hungary mnamo mwezi Septemba.

Akiwa mzaliwa wa eneo la Buenos Aires , Argentina 1966, Papa francis alipoteza upande mmoja wa pafu lake la kulia akiwa na umri wa miaka 21.

Pia aliugua tatizo la nyonga na sciatica ambayo hueneza maumivu mgongoni na miguuni.

Mwaka 2014, alilazimika kukatiza hafla nyingi kutokana na tatizo la tumbo , iliripotiwa.