logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Paula Kajala ana ujauzito wa Marioo?

Marioo amefichua kuwa mpenzi wake Paula Kajala ni mja mzito.

image
na

Burudani14 July 2023 - 09:57

Muhtasari


• Marioo amefichua kuwa mpenzi wake Paula Kajala, mtoto wa mwigizaji mkongwe Fridah Kajala ni mja mzito.

Mwanamuziki wa Tanzania, Marioo amefichua kuwa mpenzi wake Paula Kajala, mtoto wa mwigizaji mkongwe Fridah Kajala ni mjamzito.

Katika mahojiano na wanahabari wa Tanzania, Mwanamuziki huyo aliunga semi za mtangazaji mmoja kutoka Tanzania, Mwijako kuwa Marioo atamuoa Kajala baada ya kumzalia mtoto. Mwajako alizungumza kwa ujasiri akisema Paula alikuwa mjamzito.

“Ngoja ajifungue kwanza, si unaona Marioo amenyamaza tukisema hiyo mambo. Mario niskize vizuri usije ukamuoa  kabla hajajifungua. Ajifungue ndio umoe nimekuambia na nsisitiza tena usioe kabla hajifungua.”  Mwijako alimsisitizia Marioo.

Marioo akionekana kukubalianana maneno ya Mwaijako alisema, “ Msemaji wa ndoa ndio anaongea , mimi siongei chochote.”

Mwijako aliongeza haikuwa sawa kwa Marioo kuzungumzia maswala ya ndoa kama bado mpenzi wake hajajifungua na ndio sababu alikuwa akizungumza kwa niaba yake.

Paula na Mario waliingia katika uhusiano wa kimapenzi mapema mwaka huu baada ya Paula kutengana na mwanamuziki Rayvanny kwa sababu zisizo fahamika.

Mwanamitindo huyo amejitokeza mara kwa mara na kuonyesha mapenzi yake kwa Mario hatharani na ata kukiri kuwa yupo tayari kukufa kwa sababu ya mapenzi yake kwa mwanamuziki Marioo.

Mpenzi huyo wa zamani wa Rayvanny alibainisha kuwa mapenzi yake ya dhati kwa Marioo yanaweza kumfanya hata kufa kwa ajili yake.

“Nampenda sana mpenzi wangu, nipo tayari hata kufa kwa ajili yake” alisema Kajala huku akijipapasa kifuani ishara ya kuonyesha mapenzi.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved