Simulizi: Nilipata mimba ya ajabu, sikuwahi lala na mwanaume wala kuwekewa mbegu!

Akiwa na miaka 16, alijisikia kuwa mgonjwa wazazi wakampeleka ospitalini alikofanyiwa vipimo na kupatikana ni mjamzito, madaktari pia walibaini kwamba ni bikira - hakuwa amefanya mapenzi tangu kuzaliwa.

Muhtasari

• "Mtoto hajawahi niuliza kuhusu babake, lakini ikifika muda atafanya hivyo, nitamwambia ukweli kwamba nilipata mimba yake bila mume,” Suzan alisema.

• "Madaktari waliposhindwa kubaini ni kwa jinsi gani nilipata mimba, babangu alinichukua kwa mganga wa kienyeji na yeye pia alisema vivyo hivyo,” Suzan alisimulia.

Mrembo asimulia jinsi alijipata ni mjamzito angali bado bikira.
MIMBA YA AJABU: Mrembo asimulia jinsi alijipata ni mjamzito angali bado bikira.
Image: Screengrab//YouTube.

Mwanamke mmoja nchini Uganda ambaye ni bikira mwenye umri wa miaka 28 amewashangaza wengi baada ya kufichua kwamba alijifungua mtoto bila ya kuguswa wala kujamiiana na mwanamume yeyote.

Namubiru Suzan kutoka wilaya ya Luweeru nchini Uganda alihadithia kwamba kipindi hicho alikuwa na miaka 16 na alijisikia vibaya na kwenda hospitalini.

Madaktari walimpima na kupata kwamba alikuwa mjamzito, jambo ambalo lilishangaza kila mtu kwani alikuwa ni bikira na hakuwahi lala na mwanamume mwingine.

“Nikiwa na miaka 16 nilijipata mjamzito, mamangu aliniuliza kuhusu ujauzito na nilikataa. .. Mtoto hajawahi niuliza kuhusu babake, lakini ikifika muda atafanya hivyo, nitamwambia ukweli kwamba nilipata mimba yake bila mume,” Suzan alisema.

Suzan anakiri kwamba hakuwahi kuwa na mwanamume na tangu kipindi hicho hadi sasa akiwa na miaka 28 bado hajawahi kutana na mwanamume na watu kijijini mwao wanamuita ‘Maria mama wa Yesu’ kutokana na hadithi yake ya kushangaza.

Wazazi wake kipindi hicho walipigwa na butwaa wasiweze kuamini kilichotokea kwa binti yao kupata mimba pasi na kushiriki ngono na mwanamume na wasiwasi wao ulidhibitishwa hospitalini.

Jambo la kushangaza Zaidi, hata madaktari walibaini kwamba hajawahi shiriki katika kitendo cha ngono na kuwa hakubakwa kwani bado alikuwa bikira mwenye mimba.

“Ilikuwa na kuchanganyikiwa kwingi mimi kuwa na mimba pasi na kufanya ngono. Kwa hiyo wakati madaktari walinifanyia uchunguzi walipata niko na mimba lakini pia walibaini kwamba nilikuwa  bikira, jambo ambalo lilimshtua kila mtu. Madaktari waliposhindwa kubaini ni kwa jinsi gani nilipata mimba, babangu alinichukua kwa mganga wa kienyeji na yeye pia alisema vivyo hivyo,” Suzan alisimulia.

Tukio hilo la kushangaza liliwaacha wengi bila majibu kwa maswali yao mengi kwani binadamu pekee anayesemakana kupata mimba pasi na kushiriki ngono ni Maria mama wa Yesu kutoka Biblia takatifu anayesemakana kupata mimba kupitia uwezo war oho mtakatifu.

Dhana mbalimbali ziliibuliwa kuhusu tukio hilo, wengine wakisema kwamba katika mto ambao wasichana hao walikuwa wanakwenda kupiga mbizi kuna wanaume walikuwa pia wanapiga mbizi kule na wengine kujichua wenyewe hivyo kuacha manii yao kwa maji.

Kisha msichana huyo alipopiga mbizi aliingiwa na manii yale na kumsababishia kupata mimba ya kimiujiza.

Kwa mujibu wa simulizi hiyo, hili halikuweza kubainika bayana lakini dhana hiyo ilichukuliwa tu hivyo mradi kuridhisha jamii na maelezo ya mimba hiyo.

Mwanamke huyo alikumbuka kwamba licha ya kuwa yeye na wazazi wake walikubali kilichotokea, majirani, jamaa na marafiki hawakuweza kutulia na wengine walikuwa wanamnyanyapaa kuwa alipata mimba akiwa na umri mchanga.

Mwanamke huyo hata hivyo alikwenda na kuanza iashara zake na baadae kupata mwanamume wa kumpenda na kuishi naye.

Na sasa, anatoa himizo kwa kina dada wengine ambao wanajipata katika hali ngumu isiyoweza kuwa na majibu.

“Wakati hilo linakupata, hufai kukata tamaa. Pata mtoto wako, mlee na mlinde. Huwezi elewa, mtoto ni Baraka na mimi sielewi kwa nini baadhi ya wasichana wanajipata wajawazito na kitu kinachokuja katika akili zao ni kuavya,” anashauri.

Mrembo huyo anasisitiza kwamba kitendawili kigumu ako nacho ni kutegua baba wa mtoto wake ni nani, wala hapati picha siku mtoto wake atamuuliza swali hilo.

“Ni kitendawili kigumu sana japo mwanangu bado hajaniuliza swali hilo lakini nina uhakika ataniuliza siku moja. Siwezi sema ni nani alinipa ujauzito kwa sababu wanaume wengi walikuwa wanapiga mbizi katika mto tulikokuwa tunaishi. Nimejaribu kwenda pale mara kadhaa kuona kama naweza pata mwanamume mwenye anafanana na mtoto wangu, sijawahi mpata mwenye wanafanana,” alisema.

“Nikaweza kumpata mwenye anafanana na mwanangu nitamuuliza tufanye vipimo vya DNA na hata kama hatanipa msaada wa malezi mimi nitafarijika kwamba mwanangu atakuwa na mtu wa kuita baba. Sasa mwanangu amekua ana miaka 11 na anasoma shuleni, babake akija siwezi mruhusu kuchukua mwanangu bali nitakubali tu kunipa msaada wa malezi,” aliongeza.