logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwa nini andropause, "ukomo wa uzazi kwa wanaume," hautambuliwi kimatibabu?

Wanaume hawana uzoefu wa jambo kama la kumaliza hedhi, kama wanawake wanavyofanya.

image
na Davis Ojiambo

Habari28 November 2023 - 05:38

Muhtasari


  • • kuna visa vinavyotokana na msururu wa matukio ambavyo huweza kusababisha kushuka kwa homoni za kiume.
Viwango vya chini vya testosterone vinaweza kutokea na kusababisha athari hususan katika afya ya ngono.

Maumbile ya kibaiolojia ya wanaume na wanawake huwa hayana mfumo unaofanana kila wakati. Mfano wa hili ni mabadiliko ya baadhi ya homoni za kawaida.

Kwa upande wa vitu kama vile homoni za estrojeni hatua kwa hatua huacha kuzalishwa katikati ya muongo wa tano wa maisha.

Kwa wakati huu, unaojulikana kama ukomo wa hedhi, mwanamke hupoteza uwezo wa kuzalisha mayai ya uzazi kutoka kwenye ovari na kupata hedhi na kuwa vigumu kupata mimba kwa njia za asili kwasabau hupoteza uwezo wa kuzalisha mayai ya uzazi.

Kwa upande mwingine kwa binadamu hakuna mchakato unaofanana. Homoni ya kiume inayohusishwa na uzalishaji wa mbegu za kiume (testosterone ) miongoni mwa kazi zake nyingine, huonekana kuendelea kubaki mara kwa mara katika maisha yote ya mwanamume , hata baada ya kufikia umri wa miaka 50, 60 au 70.

Ikiwa tunafuata hoja hii, neno "andropause" - ambalo limepata umaarufu kuelezea aina ya "kufikia ukomo wa uwezo wa kuzalisha wa wanaume", na kupunguza uwezekano wa uzalishaji wa testosterone baada ya umri fulani - haina maana ya kimantiki, kulingana na wataalam.

Lakini ni muhimu kufikiria kuwa: kuna visa vinavyotokana na msururu wa matukio ambavyo huweza kusababisha kushuka kwa homoni za kiume testosterone na hivyo kusababisha athari mbaya ambazo hazikutarajiwa.

Hali hizi, zinazojulikana kama hypogonadism (ukomo wa uzazi wa kiume), zina vigezo vya uchunguzi na matibabu.

Hivi karibuni, miongozo ya usimamizi wa upungufu wa homoni za kiume imepitia mfululizo wa mabadiliko, kwa lengo la kuzuia matumizi ya kupita kiasi ya testosterone kama steroid ya anabolic, kwa madhumuni ya urembo kwa wanaume au wanawake

Hadithi ya andropause

"Maelezo yoyote ya andropause lazima yaanze na ukweli kwamba haipo," anasema Dk Alexandre Hohl, rais wa zamani wa Jumuiya ya Brazil ya wataalamu wa magonjwa mbali mbali ya homoni (SBEm).

"Neno hili ni neologism lilibuniwa kutokana na dhana ya ukomo wa uzazi, asili yake ikiwa ni kutoka lugha ya Kilatini: linahusiana na usumbufu unaotokana na ukomo wa hedhi. Kwa maneno mengine, kumaliza hedhi ni kukomesha hedhi" , anaelezea.

"Kutoka hapo, mtu alikuwa na wazo la bahati mbaya la kuunda dhana ya andropause, ambalo linasababisha tu utambuzi wa makosa na matumizi yasiyo ya lazima ya testosterone," analalamika Dk Hohl.

Daktari Luiz Otávio Torres, katibu mkuu wa Jumuiya ya madaktari wa maradhi ya kibofu cha mkojo ya Brazil, anakubaliana.

Dkt Hohl anaeleza kuwa katika maisha yao yote, wanaume hawana uzoefu wa jambo kama la kumaliza hedhi, kama wanawake wanavyofanya.

"Kibaiolojia , wanaume hupungukiwa kwa taratibu na uzalishaji wa homoni za kiume za kuzalisha testosterone, hasa baada ya umri wa miaka 40 au 50. Lakini kama ni mtu mzima mwenye afya, huenda akafikia miaka yake ya 60, 70 au hata 80 na viwango vya kutosha vya homoni hii, bila ya haja ya kuingilia kati au kuibadilisha," anaelezea.

Upungufu huu wa taratibu na wa asili katika homoni ya kiume, ambayo huzalishwa na korodani, hutokea kwa kiwango cha asilimia 1.2 kwa mwaka kutoka umri wa miaka 40 au 45.

"Kwa maneno mengine, wanaume wanaweza hata kuwa na kupungua kwa testosterone, lakini hawaachi kuzalisha homoni kama wanawake," Torres anaelezea kwa kifupi.

Lakini kushuka kwa homoni hii kunaweza kuongezeka kutokana na sababu nyingine , kama vile ugonjwa wa kisukari au kuongezeka kwa unene wa kupindukia wa mwili.

Kwa watu wenye magonjwa haya au mengine sugu, viwango vya testosterone vinaweza kupungua zaidi kuliko ilivyotarajiwa. Hali hii inaitwa hypogonadism ya kiume.

Sababu nyingine zinazoweza kusababisha kupungua kwa homoni hii ni pamoja na magonjwa yanayoathiri tezi ya pituitary (muundo wa ubongo unaohusika na kudhibiti uzalishaji wa testosterone katika korodani) au viungo vya uzazi vya kiume vyenyewe.

Pia kuna watu ambao, kwa sababu za maumbile, hawapitii michakato inayohusiana na kubalehe na matokeo yake hawakupata ukuaji katika uume wao, korodani na nywele za siri.

Lakini je ni wakati gani madaktari wanashuku hypogonadism?

Hohl anasisitiza kwamba kulingana na miongozo ya hivi karibuni, upimaji wa viwango vya testosterone hauipaswi kuwa sehemu ya vipimo vya kawaida.

"Hakuna sababu ya kujumuisha tathmini ya homoni hii katika uchunguzi wa afya," anaamini.

"Hali hii inakuwa na umuhimu wa kufuatiliwa kimatibabu wakati inaambatana na dalili zake ," anaongeza Torres.

Kwa hiyo, kunakuwa na uwezekano wa ‘’hypogonadism’’ ya kiume iwapo kuna uwepo wa kimatibabu , ambayo yanaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu.

"La kwanza ni pale mwanaume anapoletwa ofisini kwetu akiwa na umri wa miaka ishirini na zaidi na kubaini kuwa uume wake na korodani havijakua. Huu ni utambuzi rahisi kutambua, "anaelezea mtaalamu wa magonjwa ya homoni.

La pili ni kuhusiana na uwepo wa dalili ya evocative sana. "Huu ni usumbufu unaohusiana na nyanja ya ngono, kama vile matatizo ya ujenzi/ au kupungua kwa hamu ya ngono," anaelezea Dk Torres.

"Baadhi pia huripoti kupungua kwa orgasm au ugumu wa kumwaga.

Masuala haya ya afya ya ngono yanaweza au kutoweza kuambatana na usumbufu mwingine, kama vile kupata majeraha madogo, kupatwa na joto la mwili kupita kiasi.

"Hali tete zaidi inahusu kundi la tatu, ambalo kuna mashaka kidogo na hatari kubwa ya unyanyasaji wakati wa kuagiza testosterone," anatathmini Hohl.

Hakika, kushuka kwa testosterone katika hali hizi inaweza kuathiri idadi kubwa ya wanaume.

"Tunazungumzia hapa juu ya kuvunjika moyo, uchovu, hali mbaya, matatizo ya usingizi, udhaifu, kupoteza misuli, kuongezeka kwa ukubwa wa kiuno, na kuongezeka kwa uzito...", anaorodhesha daktari.

Kwahivyo ni muhimu kupitia mashauriano mazuri, wakati ambapo mtaalamu wa huduma ya afya anatathmini mfululizo wa dalili na kufanya vipimo fulani vya damu.

"Upimaji wa Testosterone unapaswa kufanyika kwa wanaume ambao wana historia ya ugonjwa wa pituitary au testicular, matumizi yanayoendelea ya opioids au corticosteroids, kupoteza uzito unaohusishwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU), utasa, kupungua kwa hamu ya tendo la ngono au kushindwa kusimama kwa uume", anaelezea rais wa zamani wa SBEm.

Swali la ni kiasi gani cha homoni za kiume zinaonyesha upungufu au hali ya kawaida ni suala la mjadala mkubwa ndani ya jamii za matibabu.

Kwa ujumla, wataalam wanasema kupungua kwa thamani ya homoni hadi chini ya kipimo cha 300ng / dl (nanograms kwa deciliter) kunaweza kupelekea uhitaji homoni mbadala.

Haitoshi kuchukua kipimo cha damu, kuzipeleka maabara na kufanya uamuzi kulingana na matokeo haya: sampuli lazima zichukuliwe asubuhi (kati ya saa kumi na mbili na saa nne asubuhi ), wakati testosterone ya uzalishaji zinafikia kiwango chake cha juu kwa siku.

Hohl anasisitiza kuwa uingizwaji wa testosterone una maana tu wakati homoni hii iko chini katika mwili.

"Kwa mtazamo wa afya, haina tofauti ikiwa mtu ana kiwango cha 500 ng / dl ya testosterone na huongeza hadi 600 au 800. Haimaanishi anakuwa mwanaume zaidi iwapo ana ongezeko hili," anaelezea.

"Kwa upande mwingine, ikiwa ana ng/dl 250 na huenda hadi 500, kwa mfano, afya yake inaweza kuimarika sana," analinganisha.

Kukimbilia Anabolic steroid

Uangalifu huu wote katika kutoa homoni ya kiume ni kwa sababu matumizi yake yamekuwa yameongezeka zaidi katika miaka ya hivi karibuni. Watu wengi wameanza kuitumia kwa madhumuni ya urembo, kama vile kuongeza ukubwa wa misuli na kupunguza uzito wa mwili.

Ripoti iliyochapishwa na Folha de S.Paulo inaonyesha ongezeko la 45% katika mauzo ya matoleo ya dawa ya testosterone kati ya 2019 na 2021 nchini Brazil.

Matumizi ya bidhaa katika muktadha huu pia ilikuwa mada ya azimio lililochapishwa na Baraza la Shirikisho la Dawa (CFM) mwezi Aprili mwaka jana.

Katika maandishi haya, chombo hicho kinakataza "matumizi ya androgenic na anabolic steroids kwa madhumuni ya urembo, faida ya misuli na uboreshaji wa utendaji michezo."

"Matibabu ya uingizwaji wa homoni yanafaa kutolewa kwa watu wenye upungufu maalum uliothibitishwa, au upungufu uliogunduliwa ambapo tiba hiyo inatoa faida zilizothibitishwa kisayansi," inabainisha taasisi ya udhibiti wa viwango.

Hohl anaelezea kuwa, kutokana na kanuni mpya, matumizi ya matibabu ya testosterone ni madogo kwa makundi matatu.

Kwanza, wanaume wanaosumbuliwa na hypogonagism. Pili, kwa wanawake wanaosumbuliwa na shida ya hamu ya ngono. Na, tatu, kwa wanaume waliobadilisha jinsia, kwa lengo la kubadilisha jinsia zao.

Anaamini kwamba, ikiwa inatumiwa kwa kufuata vigezo vilivyowekwa, testosterone ni bora na haidhuru afya.

"Kwa maana hii, tunapaswa pia kuwa na wasiwasi juu viwango vya chini vya homoni hii. Watu wengi wana chuki na hofu kuhusu matumizi ya testosterone, kwa sababu wanafikiri kuwa hutumiwa tu na kwamba ni hatari kwa korodani, "anasisitiza Bw. Hohl.

"Kutokana na hali hiyo, wanaume wengi ambao wanashauriwa kufanyiwa matibabu hawatafuti ushauri wa mtaalamu wa afya," anasema.

"Kwa bahati mbaya, wanaume kwa ujumla hawaendi kwa daktari mara kwa mara kama wanawake wanavyokwenda kwa madakatari wa uzazi wa wanawake," anasema Torres.

"Kwa hiyo, wakati tuna fursa ya kuwachunguza wagonjwa wetu kuhusu afya yao ya ngono, hii inaweza kuwa njia ya kuanza uchunguzi juu ya kushuka kwa viwango vyao vya testosterone," anahitimisha daktari.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved