Ni nini hufanyika mama wajawazito na wanaonyonyesha wanapokula samaki?

Wanasayansi na wataalam wanasema kwamba wanawake wajawazito wanapaswa kula kitoweo hiki kwa kiasi kidogo

Muhtasari

•Chembechembe za PCB kwenye maziwa na maji safi, zinapatikana kuwa zinamezwa na samaki wengi sana.

•Huduma ya Kitaifa ya Afya nchini Uingereza inawashauri wanawake wajawazito nchini humo kupunguza ulaji wao wa samaki kutokana na kuwa na PCB nyingi.

Image: BBC

Wataalamu wa lishe wanasema samaki ni chakula kizuri kwa afya. Lakini sasa wanasayansi na wataalam wanasema kwamba wanawake wajawazito wanapaswa kula kitoweo hiki kwa kiasi kidogo.

Wakati ambapo hifadhi ya samaki inapungua duniani kote, suala la ni kiasi gani cha ulaji wa samani kina manufaa makubwa kwa afya limekuwa suala la mjadala.

Wakati kitoweo hiki kinapatikana kwa wingi kuna wasiwasi juu ya ongezeko la mabaki ya kaboni katika viumbe vya baharini .. swali la ni kiasi gani ni muhimu kula samaki imeanza kujitokeza.

Kulingana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, hifadhi ya samaki imepungua hadi asilimia 66 ikilinganishwa na 1974.

Hata hivyo, wataalam wanapendekeza kwamba ni bora kwa mama wajawazito na wanaonyonyesha kupunguza matumizi ya baadhi ya viumbe vya baharini kama samaki.

Wataalamu wanatoa ushauri huu kwani kuna kiwango kikubwa cha zebaki na kemikali nyinginezo kwenye maji ya bahari.

Je, ni vyema au vibaya kula amaki halisi?

Image: BBC

Upatikana wa chuma katika samaki

Katika miongo michache iliyopita, kumekuwa na wasiwasi kwamba athari za uchafuzi wa bahari wa taka za vyuma zinazoingia kwenye maji ya bahari huathiri sana samaki.

Ingawa takataka za kaboni zinazotengenezwa na bindamu -polychlorinated biphenyls (PCBs) zinazotoka kwa taka za viwandani zimepigwa marufuku tangu miaka ya 1980, imegundulika kuwa zinaendelea kurundikana katika ardhi na maji.

Wataalamu walihitimisha kuwa huathiri sehemu mbalimbali za mwili, kuanzia kwenye ubongo wa binadamu hadi kwenye mfumo wa kinga.

Chembechembe za PCB kwenye maziwa na maji safi, zinapatikana kuwa zinamezwa na samaki wengi sana.

Jonathan Napier, mkurugenzi wa Utafiti wa Rothamsted nchini Uingereza, alisema kuwa njia ya kuondoa madhara yao ni kuepuka kula vyakula vilivyo vyenye kiwangi cha juu cha samaki.

"Aina hizi za mabaki ya hatari ni nyingi kwa wanyama ambao wanadamu huwinda na kula," aliongeza. Ndiyo maana anaamini kwamba samaki wanaokuzwa kwenye madimbwi ni bora kwa kiasi fulani kuliko samaki wanaopatikana baharini.

Hata hivyo, mabwawa ya samaki pia yanahusika na uchafuzi mwingi wa maji ya bahari. Kwa vile uchafu wa madimbwi hayo huchanganyika baharini kwa kiwango kikubwa, magonjwa yote yanayozaliwa hapa yanaathiri pia afya ya samaki wa baharini.

Huduma ya Kitaifa ya Afya nchini Uingereza inawashauri wanawake wajawazito nchini humo kupunguza ulaji wao wa samaki kutokana na kuwa na PCB nyingi.

Wataalamu wanasema kuwa mabaki ya zebaki ambayo huingia ndani ya samaki kupitia maji na kisha ndani ya tumbo la mwanadamu huathiri ukuaji wa mwanadamu.

Zebaki inajulikana kama moja ya chuma vyuma vinavyosababisha saratani. Pia wataalamu wanasema kuwa zebaki ndio chanzo cha kisukari na matatizo ya moyo.

Utafiti umehitimisha kuwa asilimia 78 ya zebaki huingia kwenye mwili wa binadamu kupitia samaki, ingawa kuna asilimia ndogo kwenye mboga. Ndiyo maana Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) imewashauri wanawake wajawazito kupunguza ulaji wa samaki aina ya jodari na halibut.

Wanasayansi wana wasiwasi kwamba kadiri halijoto duniani inavyoongezeka, uwezekano wa zebaki kuchanganyika katika maji utaongezeka, na kadiri eneo la Aktiki linapoyeyuka, mabaki ya zebaki baharini yataongezeka

Samaki wa baharini dhidi ya samaki wa maji baridi

Utafiti umehitimisha kwamba asidi ya mafuta kama vile eicosapentaenoic (EPA), asidi ya docosahexaenoic (DHA) na omega-3 ya baharini huwajibika kwa matatizo ya moyo ikiwa unakula samaki wenye mafuta kama lax, tuna, sardini na makrill.

Hata hivyo, utafiti bado unafanywa kuhusu ikiwa asidi ya mafuta ya omega-3 kutoka kwa mimea ni sawa na asidi ya mafuta kutoka kwa viumbe vya baharini.

"EPA na DHA zina jukumu muhimu katika kimetaboliki ya binadamu. Lakini ni makosa kufikiria kuwa wao ni muhimu,” amesema Napier.

DHA iko juu katika ubongo wa binadamu, retina, na seli zingine. Pamoja na EPA, inasaidia kudhibiti hali ya uchochezi katika mwili. Moto huu husababisha magonjwa kama vile magonjwa ya moyo, saratani na kisukari.

"Watu wanaotumia zaidi EPA na vyakula vya DHA kwa ujumla wana matatizo kidogo ya magonjwa. Hasa magonjwa ya moyo ni kidogo," alisema Profesa Philip Calder, ambaye anafanya kazi katika Chuo Kikuu cha Southampton nchini Uingereza.

Njia moja ya kupunguza madhara ya zebaki wakati wa kumeza omega-3s ni kuchukua mafuta ya samaki. Lakini utafiti wa Shirika la Afya Duniani una matokeo mchanganyiko. Utafiti huu ulihitimisha kuwa athari za kuuchakata samakisi sawa na ulaji wa mafuta ya samaki.

Leigh Hooper, msomi katika Chuo Kikuu cha East Anglia, alifichua kwamba uchunguzi mmoja uligundua kwamba kati ya watu 334 waliotumia omega-3 kwa miaka minne hadi mitano mfululizo, hakuna aliyekufa kwa matatizo ya moyo.

Athari za ulaji wa samaki kwa afya ya kila mtu na kiwango ambacho wanabadilishwa kuwa EPA na DHA hutofautiana kati ya mtu na mtu.

Kulingana na Philip Calder, vinasaba pia huathiriwa na mtindo wa maisha wa mtu na vyakula vingine anavyokula.

Wataalamu wanasema kuwa faida za kula samaki hutegemea mahali ambapo samaki hufugwa.

Hakuna uhaba wa omega-3s katika bahari ya kina. Husafirishwa kutoka kwa mimea hadi kwa samaki wadogo, kutoka kwa samaki wadogo hadi samaki wakubwa, kutoka kwa samaki wakubwa hadi kwa wanadamu. Lakini, agizo hili halipo katika samaki tunaowafuga. “Samaki tunaofuga kwenye mabwawa hula chakula anachoweka mkulima na kukua,” alisema Napier.

Zaidi ya hayo, samaki wanaofugwa hula samaki wadogo wa aina moja. Lakini samaki wanaokulia katika mito na bahari hula aina tofauti za samaki na kukua.

Utafiti uliofanywa mnamo 2016 uligundua kuwa asilimia ya EPA na DHA katika samaki imepungua karibu nusu katika muongo mmoja. Napier alifichua kuwa omega-3 nyingi zaidi zilipatikana katika samaki wanaofugwa kuliko samaki wa baharini.

Lishe kwa ubongo

Pamoja na omega-3, samaki wameonekana kuwa na virutubisho vingi vinavyopunguza maambukizi. Pia inaaminika kuwa kula samaki hufanya ubongo kuwa hai.

Wanasayansi wamegundua kuwa omega-3 inahusiana na uwezo wa ubongo kufanya kazi kwa kasi. Kula samaki waliopikwa pia kumezingatiwa kuongeza ukubwa wa ubongo.

Kama sehemu ya utafiti kuhusu athari za virutubishi kutoka kwa samaki kwenye ubongo, watu 163 wenye umri wa zaidi ya miaka 70 walifanyiwa uchunguzi wa MRI.

Hata hivyo, akili za wale waliokula samaki kila wiki zilionekana kuwa kubwa zaidi ikilinganishwa na wale ambao hawakula samaki. Hasa mageuzi ya maeneo ya ubongo ambayo hufanya kazi kwenye kumbukumbu na akili ni ya juu.

Wanasayansi wanasema kwamba kuna faida nyingine katika kula samaki. "Ikiwa tunakula samaki wengi, hatutaki kula vyakula vingine," Hooper alisema.

Calder alisema pamoja na kwamba hakuna utafiti wa kutosha juu ya hatari kwa wale ambao hawali samaki, kuna faida nyingi kwa wale wanaokula. Omega-3 ni nzuri kwa afya, anasema, haswa kwa moyo.

Ikiwa sivyo, suala la kweli ni jinsi samaki tunayokula walivyo na afya. "Kulima mwani kunaweza kuharakisha utafiti katika kuchimba omega-3s," Calder alisema.

Kupata na kula aina nzuri ya samaki kunaweza kuwa na manufaa kwa kiasi fulani. Jumuiya ya Uhifadhi wa Baharini imeandaa orodha ya aina gani za samaki ni nzuri.

Aina 50 za samaki kati ya spishi 133 za samaki zimetajwa kuwa nzuri katika orodha hii. Tuna bahati kwetu, orodha hii inajumuisha samaki maarufu kama lax, kamba, chewa, makrill, oyster na halibut.

Image: BBC

Hata hivyo, mabwawa ya samaki pia yanahusika na uchafuzi mwingi wa maji ya bahari. Kwa vile uchafu wa madimbwi hayo huchanganyika baharini kwa kiwango kikubwa, magonjwa yote yanayozaliwa hapa yanaathiri pia afya ya samaki wa baharini.

Huduma ya Kitaifa ya Afya nchini Uingereza inawashauri wanawake wajawazito nchini humo kupunguza ulaji wao wa samaki kutokana na kuwa na PCB nyingi.

Wataalamu wanasema kuwa mabaki ya zebaki ambayo huingia ndani ya samaki kupitia maji na kisha ndani ya tumbo la mwanadamu huathiri ukuaji wa mwanadamu.

Zebaki inajulikana kama moja ya chuma vyuma vinavyosababisha saratani. Pia wataalamu wanasema kuwa zebaki ndio chanzo cha kisukari na matatizo ya moyo.

Utafiti umehitimisha kuwa asilimia 78 ya zebaki huingia kwenye mwili wa binadamu kupitia samaki, ingawa kuna asilimia ndogo kwenye mboga. Ndiyo maana Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) imewashauri wanawake wajawazito kupunguza ulaji wa samaki aina ya jodari na halibut.

Wanasayansi wana wasiwasi kwamba kadiri halijoto duniani inavyoongezeka, uwezekano wa zebaki kuchanganyika katika maji utaongezeka, na kadiri eneo la Aktiki linapoyeyuka, mabaki ya zebaki baharini yataongezeka.