Jinsi wakenya wanavyopaza sauti zao dhidi ya ushirikiano wa Serikali na IMF

Baadhi ya Vijana wamedai kuwa mashirika kama vile IMF pamoja na World Bank yamekuwa yakiingilia kati masuala ya Kenya huku Mswada wa Fedha 2024 ukiwa umeundwa na IMF

Muhtasari

•Vifo vya vijana wenye umri wa makamu vimekuwa vikishuhudiwa kila kukicha vingine vikiwa ni vya kutatanisha na kutamausha ghaya isiyo kifani.

•Wakenya wa Diaspora hasa Marekani walichukua hatua na kuandamana kwenye makao makuu ya IMF pale Washington DC ambapo walikashifu na kushutumu IMF kwa kuleta hali ya patashika nchini Kenya.

Kijana abeba kibango ili kupitisha ujumbe kuwa hata wakitekwa nyara hawatatishwa
Image: JOSEPH OMBATI

Baadhi  ya wananchi wameibua mdahalo mkali kuelekeza kwa serikali kufuatia matumizi ya nguvu zaidi na serikali katika kuwatawanya waandamanaji.Vilevile, baadhi ya wakenya wa diaspora wamelaumu serikali kutokana na ushirikiano wao na IMF ambao umevuruga amani katika taifa la Kenya. 

Hali ya kwikwi na simanzi imezidi kutanda katika taifa la Kenya huku baadhi ya vijana wakitekwa nyara mchana peupe wakiwa kwenye maandamano ya kpinga serikali.

Mbali na hayo, vifo vya vijana wenye umri wa makamu vimekuwa vikishuhudiwa kila kukicha vingine vikiwa ni vya kutatanisha na kutamausha ghaya isiyo kifani.

 Kisa kilicho waacha wengi vinywa wazi kwa kubung’aa na kuduwaa ni kile cha Kware ambapo vipande vya miili iliyokatwakatwa iliopolewa kutoka kwenye sehemu ya kutua taka.

Katika maandamano ya hivi punde mnamo Alhamisi, mwanaharakati Boniface Mwangi alikamatwa akiwa anaandamana huku akiwa pamoja na ninaye marehemu Evans Kiratu aliyefariki kwenye ghasia za maandamano.

Vilevile, mwanaharakati Shadrack Kiprono almaarufu SHAD KHALIF alikamatwa kwa mara ya pili tena huku asijulikane alipopelekwa.

“Shadrack Kiprono yuko wapi na GOK inamficha wapi baada ya kutekwa mchana kweupe? Haikubaliki kwamba polisi hawawezi kuzingatia utawala wa sheria. #FreeShadKhalif!” Aliuliza Kevlan kwenye jukwaa lake la mtandao wa X.

Yakini hali ya hofu imezidi kuchacha katka maeneo mbalimbali ya nchi huku wananchi wakihofia usalama na ukuaji wao kwanimagari yasiyo na sahani ya nambari yameonekana yakipita katika barabara nyingi kuu jijini Nairobi kinyume na sheria.

Magari haya yanadaiwa kuhusishwa na utekaji nyara wa adinasi wengi jijini nairbi huku wasijulikane walipopelekwa.

“Hatuombi, mnahitaji kumwachilia Shadrack Kiprono na wote waliotekwa nyara jana kinyume na sheria.” Alidokeza Arnold pale X.

Vilevile, wanahabari walichukua hatua na kuingia kwenye jiji la Nairobi ili kuandamana dhidi ya matumizi mabaya ya nguvu zaidi na askari huku kupigwa risasi kwa mwanahabari Catherine Wanjeri na kukamatwa kimabavu kwa mwanahabari Macharia Gaitho  kukizidi kuibua maswali chungu nzima vilevile kupandisha wananchi mori.

Ama kweli Jamhuri huru ya Kenya si huru tena kwani madai ya wananchi hasa vijana wamedai kuwa mashirika kama vile IMF pamoja na World Bank yamekuwa yakiingilia kati masuala ya Kenya huku Mswada wa Fedha 2024 ukiwa umeundwa na IMF wala sio wabunge wa  Kenya.

Mswada huo kutokana na utata wake, ulizusha hamaki miongoni mwa vijana huku wabunge 204 wakiuidhinisha kupita kiasi cha kufanya vijana hao hao kujipiga msasa na kuingia kwenye maandamano ambayo yaligharimu mabilioni ya ngwenje.

Hakika viongozi wamepaswa kusimama kidete  na kukashifu vitendo vya kiholela na uhayawani huu huku visa kama hivi vikizidi kukithiri ndani ya taifa la Kenya.

Wakenya wa Diaspora hasa Marekani walichukua hatua na kuandamana kwenye makao makuu ya IMF pale Washington DC ambapo walikashifu na kushutumu IMF kwa kuleta hali ya patashika nchini Kenya.

Vilevile walilaumu serikali kwa kushirikiana na IMF katika kuzusha mtafaruku na vurugu miongoni mwa wananchi  mwa wananchi wa Kenya huku maafa, majeraha, uharibifu wa mali pamoja na utekaji nyara wa wananchi yakizidi kuripotiwa.