logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mbinu 6 za kuepuka uchovu na maumivu ya 'hangover' baada ya kutumia vilevi

Tumekusanya baadhi ya ukweli wa kisayansi kuhusu pombe, ulevi na athari zake au hangover.

image
na BBC NEWS

Makala02 January 2025 - 07:55

Muhtasari


  • Kupoteza kumbukumbu, maumivu ya kichwa, uchovu na kichefuchefu, pamoja na njaa ya ghafla ni dalili hizo zinaweza kuelezea matatizo makubwa ya afya.
  • Pombe huwafanya baadhi ya watu kuwa wazimu, idadi ndogo ya watu hutumbukia katika hali ya huzuni, wakati wengi hujizungumzisha.
Njia za kuepuka hangover

Maumivu ya kichwa yanayotokana na unywaji wa divai nyekundu, vinywaji vyenye mchanganyiko na tiba za uchovu wa wa maumivu unaotokana na unywaji wa vilevi al maarufu hangover, ni miongoni mwa mambo unayopaswa kujua kuyahusu hali wakati wa likizo.

Kupoteza kumbukumbu, maumivu ya kichwa, uchovu na kichefuchefu, pamoja na njaa ya ghafla ni dalili hizo zinaweza kuelezea matatizo makubwa ya afya. Lakini ukweli ni kwamba mara nyingi huwa ni 'hangover' yaani athari zisizofurahisha za baada ya unywaji wa vileo.

Baada ya usiku wa kula sumu (pombe) inayopendwa na wanadamu, mamilioni ya watu huamka wakiugulia mkesha wa Mwaka Mpya na kushangaa walichokifanya jana usiku.

Ili kujibu swali hili, tumekusanya baadhi ya ukweli wa kisayansi kuhusu pombe, ulevi na athari zake au hangover.

Mvinyo nyekundu inaumiza sana kichwa

Linapokuja suala la maumivu ya kichwa ya pombe, divai nyekundu inaweza kukufanya athari mbaya. Uhusiano huu ulijulikana hata kwa Warumi zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Kwa muda mrefu ilifikiriwa kuwa sulfite ilisababisha maumivu, lakini divai nyeupe pia inayo, na haisababishi dalili zisizofurahisha kama divai nyekundu.

Kulingana na utafiti wa hivi karibuni wa wanasayansi katika Chuo Kikuu cha California, Davis, usumbufu huu unaweza kuwa unatokana na kiungo kiitwacho quercetin, ambacho kinapatikana kwa wingi kwenye ngozi ya zabibu nyekundu.

Kinyume na imani maarufu, kuchanganya vinywaji hakutakufanya ulewe zaidi - ni kiasi unachokunywa ambacho ni muhimu.

Ethanoli katika pombe kwa kawaida hubadilishwa mwilini kuwa asetaldehyde, ambayo huvunjwa kuwa acetate na kimeng'enya cha ALDH.

Wakati mwingine sio aina ya pombe ambayo ni muhimu, lakini jinsi mwili wetu unavyoipokea.

Kwa watu wengine, enzymes au vimeng'enyo havifanyi kazi kwa ufanisi, na kiwango cha acetaldehyde hatari huongezeka. Kwasababu ya hili, mtu hupata maumivu ya kichwa kutokana na mvinyo mwekundu.

...lakini nyekundu pia ina faida zake

Wazo kwamba glasi ya divai nyekundu inaweza kuwa na faida lilijitokeza katika miaka ya 1970. Wakati huo, tafiti zilionyesha kwamba Wafaransa walikuwa na hatari ndogo ya ugonjwa wa moyo, ingawa walikula mafuta mengi yaliyojaa.

Wanasayansi waliiita "kitendawili cha Ufaransa", na bado inawashangaza watafiti.

Baadaye, wanasayansi walifikia makubaliano kwamba kiasi cha wastani cha pombe kina manufaa zaidi kuliko kuacha kabisa. Lakini leo wanasayansi wanaamini kwamba data hizi zinaweza kuwa mbaya. Baada ya yote, watu wengine wanaweza kujiepusha na pombe kwasababu ya shida zingine za kiafya.

Uchunguzi zaidi ulijaribu kujua ikiwa divai nyekundu kweli humlinda mtu dhidi ya ugonjwa wa moyo.

Utafiti uliofanywa nchini China uligundua kuwa kadiri watu wanavyokunywa zaidi ndivyo wanavyokuwa na uwezekano mkubwa wa kupata shinikizo la damu na hatari ya kiharusi.

Lakini kuna upande mwenyine : wakati hatari ya kiharusi huongezeka, hatari ya kiharusi hakitokei kwa wanywaji . Inaonekana kwamba kuna kitu katika pombe kinachotulinda.

Kusubiri kunaweza kukufanya ulewe zaidi

Pombe huathiri watu kwa njia tofauti sana. Huwafanya baadhi ya watu kuwa wazimu, idadi ndogo ya watu hutumbukia katika hali ya huzuni, wakati wengi hujizungumzisha.

Kama vile mwandishi wa sayansi David Robson aelezavyo katika kitabu chake The Expectation Effect, madhara ya kileo si kemikali tu. Kwakweli, matarajio ya kijamii pia huathiri kile pombe inachotufanyia.

Katika jaribio moja maarufu, watafiti walijaribu kupima jinsi mtazamo wa kiasi ambacho watu wamekunywa kinavyoathiri tabia yao ya fujo.

Katika kipindi cha majaribio, washiriki walipewa vinywaji ambavyo, kama watafiti walivyowaeleza, vilikuwa na pombe nyingi, pombe kidogo au hakuna kabisa. Kwa kweli, kiasi cha pombe katika glasi kilikuwa sawa.

Ilibadilika kuwa wale ambao walidhani walikuwa wamekunywa zaidi walitenda kwa ukali zaidi. Watafiti walipima hili kwa kiasi cha mchuzi wa moto ambao washiriki waliongeza kwenye sahani.

Hatahivyo, kutarajia ulevi pia inaweza kuchochea kiwango chako cha ulevi.

Katika utafiti mwingine, watu ambao waliambiwa walikunywa vodka na kinywaji cha kuongeza nguvu cha Red Bull walihisi kulewa zaidi kuliko wale ambao waliambiwa walipewa "cocktail ya vodka" au "cocktail ya matunda ya kigeni."

Wale ambao waliamini kuwa pombe iliyo na kinywaji cha kuongeza nguvu ilikuwa kileo zaidi kwa kweli walihisi kulewa zaidi.

Kwahiyo, unaweza kujihakikishia madhara ya pombe kwa kunywa kidogo sana.

Hadithi ya Kuchanganya Vinywaji

Watu wanaamini kuwa sio vinywaji vyote vya pombe ni sawa katika suala la ukali wa 'hangover'.

Pombe ina athari ambayo inaweza kusababisha upungufu wa maji mwilini ikiwa haukunywa maji ya kutosha na kinywaji chako. Inajulikana pia kuwa unywaji wa pombe nyingi hudhoofisha ubora wa usingizi na hupunguza awamu ya REM (awamu ya "utendaji wa haraka wa macho").

Pia, kinywaji kikiwa na nguvu zaidi, ndivyo unavyoweza kunywa kwa muda mfupi. Kwanza kabisa, ikiwa vinywaji vinavyoficha ladha ya pombe na vyenye ladha nzuri ya kunukia.

Kawaida, mwili wetu 'huzimua' pombe haraka sana. Lakini, kama tulivyoandika hapo juu, kwa watu wengine, kwa sababu ya tofauti za maumbile, hili halifanyiki kwa ufanisi kwa baadhi.

Kiwango cha ethanol katika mwili wao kinabaki juu, na hangover itakuwa kali zaidi.

Dutu zingine katika kinywaji cha pombe zinaweza pia kuathiri jinsi unavyohisi asubuhi iliyofuata.

Ya kuu ni congeners ambayo huundwa wakati wa fermentation. Ni asetoni, mafuta ya safflower na tannins ambayo hutoa rangi na ladha ya tart kwa vinywaji kama vile whisky na divai nyekundu.

Bourbon, kwa mfano, ina congeners mara 37 zaidi kuliko vodka. Uchunguzi umeonyesha kuwa watu hupata hangover yenye nguvu baada ya kunywa bourbon kuliko baada ya kunywa vodka.

Hata hivyo, jambo muhimu zaidi ni kiasi cha pombe kinachotumiwa, na sio maudhui ya congeners ndani yake.

Wanasayansi pia walijaribu kuchunguza ikiwa kuchanganya pombe ni muhimu. Kama wazo kwamba bia ni nzuri kabla ya divai, na kinyume chake ni mbaya, au ushauri wa kutochanganya kamwe vinywaji vya zabibu na nafaka.

Utafiti huo uligundua kuwa kuchanganya vitu kwa mpangilio wowote haukuathiri ukali wa hangover. Tena, kiashiria pekee cha ukali wa hangover ilikuwa kiasi cha ulevi.

Pia, ikiwa unachanganya vinywaji, kuna uwezekano kwamba tayari umekuwa na mengi ya kunywa.

Kwa hiyo, hitimisho ni hili - ili kuepuka hangover, kunywa kidogo.

Inaweza pia kuwa na maana kuepuka vinywaji vya rangi nyeusi.

Je, tiba za 'hangover' ina ufanisi?

Kumekuwa na njia nyingi za haraka za kujiondoa katika hali ya maumivu ya baada ya kunywa vilevi - hangover. Katika Misri ya kale, ilipendekezwa kuvaa mkufu uliotengenezwa na majani ya hamedaphna ya Alexandria, na Warumi wa kale walipendekeza kula ndege aina ya canary iliyochomwa.

Wengine hujiokoa kwa chakula cha mafuta au mchanganyiko wa kuchukiza wa mayai mabichi, juisi ya nyanya na mchuzi wa moto. Lakini hangover haisababishwi na upungufu wa virutubishi.

Uchunguzi mmoja wa utafiti uliangalia tiba nane maarufu za hangover, kutoka kwa mchanganyiko wa vyakula vyenye chachu na juisi za matunda hadi dawa.

Hakuna hata mmoja ulioonyesha uwezo wa kuathiri hangover.

Majaribio ya madawa mengine pia yameonyesha matokeo mchanganyiko. Baadhi wamesaidia na dalili maalum, kama vile uchovu na kichefuchefu, lakini hakuna ambayo imeweza kuondoa dalili zote za hangover.

Juisi ya Kikorea, kwa mfano, imekuwa na ufanisi kwa watu ambao hawana maumbile ya kutegemea hangover kali.

Kujadili madhara mabaya ya pombe na marafiki itakusaidia kunywa kidogo

Inaaminika sana kwamba mayai husaidia kukabiliana na hangover, kwa sababu yana amino asidi cysteine, ambayo inaweza kupunguza baadhi ya madhara ya kiungo cha acetaldehyde.

Lakini kwa kuwa jukumu la acetaldehyde yenyewe katika hangover ni la shaka, faida inaweza kuwa sio kubwa sana. Hakika, utafiti mmoja ambao washiriki walipewa cysteine ​​​​ulipata uboreshaji mdogo katika dalili za hangover.

Inashangaza, kwasababu zisizojulikana, athari hii ilijulikana zaidi kwa wanawake kuliko wanaume.

Hatahivyo, mara nyingi, ubora wa utafiti wa aina hii sio wa kuaminika sana, kwasababu si rahisi kufanya hitimisho sahihi kuhusu ukali wa hangover.

Na kwahivyo, labda haupaswi kutumaini uponyaji wa haraka wa hangover.

Mazungumzo na marafiki huathiri kiasi cha ulevi

Uamuzi wetu, ni kiasi gani cha kunywa, mara nyingi inategemea tabia ya watu katika kampuni. Ubongo unachukua mara kwa mara ishara kutoka kwa watu wengine ili kutufahamisha kuhusu miitikio yao kwa matendo yetu.

"Kila kitu ambacho marafiki wetu hufanya hutuathiri, iwe tunatambua au la," anasema Christine Scholz, profesa msaidizi wa mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Amsterdam.

Katika utafiti wa 2019, Scholz aliwauliza wanafunzi wa Marekani ikiwa wamezungumza na mtu yeyote kuhusu uzoefu wao wa hivi majuzi wa unywaji pombe, na ikiwa mazungumzo hayo yalikuwa mazuri au mabaya.

Ilibadilika kuwa ikiwa maoni yalikuwa chanya, walikunywa pombe zaidi siku iliyofuata. Lakini ikiwa ilikuwa ni kubadilishana uzoefu mbaya, iliwahimiza kunywa kidogo katika siku zijazo.

"Wacha tuseme ninazungumza na rafiki siku iliyopita juu ya athari mbaya za pombe, lakini siku inayofuata naishia kwenye baa na watu wengine - bado nitadai kuwa mazungumzo yana athari mimi," Scholz anasema.

Kwahiyo, njia bora ya kuepuka hangover? Banal - kunywa kidogo.

Lakini kuna baadhi ya mbinu ambazo zinaweza kusaidia na hili. Kwa mfano, jadili matokeo mabaya ya kunywa na marafiki mapema. Au cheza kulingana na matarajio yako kwa kupata hali ya kufurahisha unayotafuta kupata kwa kunywa kidogo au kutokunywa pombe kabisa.

Ikiwa una sherehe mbele ambayo huwezi kuepuka pombe, jaribu kujizuia kunywa whisky na divai nyekundu.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved