Siku chache ndizo zinatenganisha umoja wa Afrika kupata kingozi mpya.
Kenya ni mojawapo ya mataifa ambayo yamewasilisha mgombeya pamoja na Madagascar na Djibouti.
Hii siyo mara ya kwanza Kenya kuwasilisha mgombea, hali sawia ilikuweko mwaka 2017 wakati rais msitaafu Uhuru Kenyatta alipomteua balozi Amina Mohamed kuwania nafasi hiyo ya kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.
Zamu hii ikiwa ya mwanasiasa mzoefu katika ulingo wa siasa na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga. kiongozi mwenye historia ya kuwani nafasi ya urais mara tano ila bahati haikusimama upande wake.
Mwaka wa 2017, Kenya ilipoteza dakika za lala salama kwa raia wa Chad Moussa Faki Mahamat ambaye pia alikuwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo.
Wakati wa kura ya awamu ya sita nchi za Uganda, Djibouti na Burundi ziliamua kubadili nia na kuchagua kutoipigia Kenya hivyo basi kura hizo tatu zikawa za muhimu kwa nchi ya Chadi. Kenya ikawekwa nje na Chad ikapishana pekee yake awamu ya mwisho na kutwa ushindi.
Mwanzoni nchi za Afrika Mashariki zilikuwa zimekubaliana na kumuidhinisha Balozi Amina Mohamed lakini ahadi hiyo haikukumbatiwa wakati wa uchanguzi.
Uganda, Burundi na Djibouti wote walimpigia Kenya katika msururu wa kwanza hivyo Mohamed akapa kura 16 dhidi ya Faki 14.
Kura zilizobaki zikawa zimegawanishwa Senegal, Botswana na Equitorial Guinea. katika msururu wa pili Chad ilipata kura 21 huku Kenya wakiongeza moja tu.
Mahamat aliendeleza ushindi wake katika msururu wa tatu kwa kura 21 dhidi 17 baada ya mataifa jirani ya Kenya kukosa kuipigia. Hata hivyo kenya ilipata uungwaji mkono tena baada wagombea wa mwisho watatu kujiondoa hivyo mgombea wa kenya akapata 26 dhidi ya Faki ambaye alipata 25.
Kura zilifikia msururu wa sita na Chadi ikavuna na kupata kura 28 dhidi ya Kenya 25. Hivyo Faki akatangazwa mshindi baada kupishana pekee yake katika raundi ya saba na kupata kura 38.
Mataifa ya SADC yalijitenga nsa uchaguzi huo baada kususia mteule wao wa Botswana alipokosa kufanikisha kuendelea mbele kwenye pambano hilo.