Historia ya siku kuu ya Redio Duniani
Tarehe 13 Februari kila mwaka ni siku ambayo ilitengwa na shirika
la umoja wa kimataifa UNESCO kama siku teule ya kusherehekea Redio Duniani kutokana na azimio la kongamano la 36 kufanyika mwaka 2011.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni kusherehekea siku ya redio duniani na
mabadiliko ya tabianchi, hii ni kuashiria kuwa redio ni kiungo muhimu katika
kupasha ujumbe unaotokana na utunzi wa mazingira yetu.
Hata hivyo tunaposherehekea siku kuu hii ya redio duniani
inatufaa kukumbuka vyema kuwa redio ni chombo cha mawasiliano ambacho hutumika
kupitisha ujumbe katika hadhira pana na lengwa.
Kwa mfano baadhi ya majukumu ambayo redio ilitumika kuweza
kupisha ujumbe ni kuelimisha, redio ilitumika katika miaka ya zamani kuelimisha
jamii katika masuala mbalimbali kama vile uongozi,kukashifu vitendo viovu kama
ufisadi na kufundisha kuhusu umuhimu wa kuishi kwa Pamoja na kushirikiana.
Vilevile redio ilitumika kama chombo cha kupasha watu na
jamii Habari na matukio yaliyokuwa yakijiri kwa mfano kuelezea jamii umuhimu wa
kushiriki katika uchaguzi,umuhimu wa kupokea chanjo na tiba iliyotolewa na
serikali na vilevile kuonya kuhusu masuala ambayo yangeleta madhara kwa jamii
au vita.
Redio kama chombo kilichotumika kuelimisha,kupasha ujumbe vilevile kutumika
kama chombo cha burudani kwa kucheza miziki kwa mshabiki miziki ambayo ilinuia
kukuza tamaduni za jamii na zile za uzalendo ambazo zililenga kuwashirikisha na
kuwaleta wananchi kwa Pamoja.
Redio kwa miaka mingi ilikuwa na imekuwa mhimili imara kwa
jamii kwa kueleza na kuwazindua wananchi kwa kuwafundisha mambo mengi
wasioyafahamu katika jamii.
Karne ya sasa kuna aina nyingi za redio ambazo zinaendeleza jukumu la kuelimisha na kuwapa
wananchi nafasi ya kujieleza ipasavyo kwa kutumia uhuru wa kujieleza katika Redio.
Katika taifa la Kenya Redio ilianzishwa mwaka wa 1927 kama
redio ya Afrika mashariki (EABC) ambapo redio hiyo ilikuwa ikitangaza Habari za
BBC kwa wazungu.
Mnamo mwaka wa 1953 baada ya vita vya pili vya dunia Redio
ya ABS ilianzishwa ikitangaza kwa lugha ya Kiswahili na Luo na baadhi ya lugha
za mama.
Hatimaye mwaka wa 1959 kituo cha KBS(Kenya Broadicasting services)
kilizinduliwa na ulipofika mwaka wa 1964 KBS ilibadilishwa jina na kuitwa VOK ambapo
ulipofika mwaka wa 1989 bunge la taifa la Kenya lilirudisha jina KBC.
Katika nchi ya Kenya kwa sasa kuna jumla ya Redio 303 kulingana
na mujibu wa mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya(CAK) ambapo kwa Redio hizo
kuna zile za binafsi, redio zinazomilikiwa na mashirika ya serikali na zile za
viwango vya Jamii.Baadhi ya redio nchini ni Radio Jambo,Radio Citizen,KBC Radio
Taifa,Radio Maisha,Radio 47 na Milele fm.