Siku kuu ya Valentino duniani 14 Februari,2025
Naam katika kulizamia swala hili na kufahamu kwa ufupi ni nini
chanzo na maana ya valentino naomba tusafiri na wewe katika kujua chimbuko
lake.
Inasemekana kuwa katika enzi ya istimari katika karne ya
tano paliondokea mtakatifu mmoja kwa jina papa Gelasius kule Roma aliyekuwa
katika hafla ya sherehe.
Inasemekana kuwa akiwa katika hafla hiyo alimuona msichana
mmoja kipofu utu ukamvaa akamkumbatia na kumwona kama mtu wa muhimu sana katika
sherehe hiyo iliyoitwa Lupakalia.
Baada ya kuonyesha upendo kwa huyo mwanadada siku hiyo licha
ya sheria iliyokua wakati huo kupinga mtumishi wa Mungu kuwa na mahusiano au
nia ya kupenda.
Siku hiyo ilibadilishwa na kuitwa mtakatifu Valentino baada
ya kufungwa jela kwa mtakatifu Valentino kutokana na kitendo cha sheria kali za
Kirumi ambazo zilikuwa kinyume na masuala ya mahusiano katika karne ya tatu.
Hatimaye watu walibadilisha fikra na kuiona siku hiyo ya 14
ambapo mfia dini mkuu wa kikristo alifanya kitendo cha kuoa, watu wakaitambua
siku hii kama siku ya upendo duniani.
Mataifa mengi duniani yakaiga mtindo huo yakaanza kusherehekea siku hio kwa namna mbalimbali kwa
kuweza kuwapa kumbukizi na fikra za kuonyesha upendo kwa wapenzi,marafiki,jamaa
na wazazi.
Baadhi ya mataifa ambayo husherehekea siku hii duniani ni
Marekani,Uingereza,Kanada, Australia,Ajentina,Ufaransa,Mekisko na Korea Kusini yakiwemo
mataifa ya Afrika.
Hata hivyo watu wanapojiandaa kusherehekea siku hii ya
Valentino mnamo Februari 14,2025 wengi watatarajia kupokea zawadi mbalimbali
yakiwemo maua na mapambo mengi sana kuashiria upendo.
Kwa hivyo kuna watu wengi ambao huwa wanasawiri siku hii
kama siku ya mapenzi kwa wale ambao wanapendana pekee ila badala yake siku hii inasitahiki kuleta
mabadiliko katika maisha ya watu wengine ili siku hii iwe ya kukumbukwa daima.
Siku ya Valentino licha ya kuwa ni siku ambayo imesheheni
upendo kuna watu ambao wanaitumia siku hii kuweza kuonyesha upendo wa dhati kwa
wazazi,wapenzi wao, Watoto mayatima,wazee na kina Mama wajane ili wahisi
umuhimu wa siku hio adhimu.
Kuna watu mbalimbali ambao watatumia siku ya Valentino
kuweza kuzuru magereza mbalimbali ili kuonyesha upendo kwa wafungwa na wagonjwa
katika hospitali mbalimbali ili kuwaombea dua ya kupona kwa Mungu, wacha iwe
siku ya heri na fanaka kwa sisi sote.
Wengi wameratibu kuweza kuzuru shule mbalimbali kwa ajili ya
kuwapokeza visodo Watoto wa kike ambao wanatoka katika Jamii zizizojiwza ili
nao waweze kuhisi wanapendwa na kuthamini siku hii ya Valentino,kutoka kwangu
mimi pia nakutakia Valentine njema.