logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Je, ni kweli Illuminati 'wanaudhibiti' ulimwengu kwa siri?

Nadharia kwamba Illuminati wanaongoza ulimwengu kwa siri na kuanzisha utaratibu mpya imekuwapo kwa miaka mingi.

image
na BBC NEWS

Makala08 March 2025 - 14:21

Muhtasari


  • Asili ya wazo hili ni tukio la kufikirika ambalo lilifanyika Ulaya katika miaka ya 1960.
  • Illuminati inasemekana kuwa nyuma ya mambo mengi yasiyojulikana, ikiwa ni pamoja na nani alimuua John F. Kennedy?

Nadharia kwamba Illuminati wanaongoza ulimwengu kwa siri na kuanzisha utaratibu mpya imekuwapo kwa miaka mingi.

Asili ya wazo hili ni tukio la kufikirika ambalo lilifanyika Ulaya katika miaka ya 1960.

'Enlightment era'ni kipindi cha kihistoria kilichotokea katika karne ya 17 na 18, kilicholeta mageuzi makubwa katika mawazo, sayansi, na jamii, hasa katika bara Ulaya.

Ujerumani inahusishwa na asili ya Illuminati.

Kulikuwa na kundi la ajabu lililoitwa Bavarians. Hii ilianza mnamo 1776.

Watu wenye elimu walikusanyika na kukosoa utaratibu na muundo wa kidini.

Kama vikundi vingine vya siri vinavyoitwa Freemasons, Illuminati inachukuliwa kuwa vya kimaendeleo.

Wakosoaji wa kihafidhina na Wakristo, hata hivyo, hawakukubali.

Walitoweka kwa muda na kurejea tena katika miaka ya 1960.

David Bramwell, ambaye amefanya utafiti kuhus Illuminati, anasema kwamba Illuminati ya sasa ni tofauti na kikundi cha uchawi cha Bavaria.

Ilikuwa wakati ambapo harakati dhidi ya mila ya kitamaduni, iliyoongozwa na falsafa ya Mashariki, ilikuwa ikienea katika ulimwengu wa Magharibi.

Wakati huo, kitabu kiitwacho 'Principia Discordia' kilichapishwa.

Riwaya hiyo inadai kwamba watu waliotaka mfumo usio na utaifa waliabudu mungu wa machafuko anayeitwa Iris.

Inaelezea maisha magumu kwa kundi linalotaka kusababisha machafuko ya kijamii.

Mmoja wa waandishi wa kitabu hicho ni Robert Anton Wilson.

Anaamini kwamba "ulimwengu umekuwa wa udikteta. Udhibiti umekuwa mkubwa sana," hivyo anatafuta kuleta mabadiliko kwa kuchochea machafuko ya kijamii.

"Aliamini kuwa mabadiliko yangeweza kuletwa kwa kutumia vyombo vya habari, kudadisi tamaduni maarufu, na kueneza habari potofu," anasema David Bramwell, ambaye ametafiti kuhusu Illuminati.

Mwandishi, pamoja na rafiki yake, walichapisha barua bandia kwenye jarida la Playboy, wakidai kuwa inatoka kwa wasomaji.

Barua hizo zinafichua kuwepo kwa kikundi cha siri kiitwacho Illuminati.

Ilikuwa ni njia ya kuwafanya watu wahoji yale waliyokuwa wakisoma na kusikia ni kweli.

Wengi walianza kuamini kuwepo kwa Illuminati.

Illuminati inasemekana kuwa nyuma ya mambo mengi yasiyojulikana, ikiwa ni pamoja na nani alimuua John F. Kennedy?

Kitabu kilichosababisha uvumi huo kuenea kilikubaliwa na kuwa ukumbi wa michezo huko Liverpool, Uingereza.

Wakati kadi za kucheza mchezo unaoitwa Illuminati zilipochapishwa mwaka wa 1975, picha zilizohusishwa kwa kawaida na kikundi hicho zilipata umaarufu.

Kwa sasa, watu wengi mashuhuri, akiwemo Jay Z na Beyonce, wanaaminika kuwa Illuminati.

Huzingatiwa sana wanapokuwa jukwaani wakitumbuiza kwa umbile la kona tatu.

Ingawa inajulikana kuwa hii sio kweli, nadharia kuhusu njama za miaka ya 1960 bado zinaendelea.

Nadharia ya uwepo wa njama inasambazwa sana kwenye tovuti kama 4chan na Reddit.

Kwa mujibu wa udadisi wa 2015 nchini Marekani, nusu ya wakazi wa nchi hiyo wanaamini angalau nadharia moja ya njama.

Kulingana na Viren Swamy, anayefanya kazi katika Chuo Kikuu cha Anglia Ruskin, watu wanaweza kuamini katika nadharia za kufanyika mipango kwa sababu mbalimbali.

Kuna wataalam wanaodhani kwamba wanaweza kuwa na aina fulani ya ugonjwa wa afya ya akili.

Wataalamu wengine wanasema kwamba watu wanaweza kupendelea jibu au maelezo rahisi kuliko uchanganuzi wa nadharia ya njama ya siri badala ya kukubali ukweli unaoondoa hali ya kujiamini.

Utafiti wa hivi karibuni unapendekeza kwamba watu walioelimika hawaamini katika nadharia za njama.

Kulingana na mtaalamu huyo, nadharia za njama hutumiwa na serikali za nchi za Asia Kusini kudhibiti idadi ya watu.

Kinyume chake, katika nchi za Magharibi, wakati watu wanahisi kuwa wamepoteza ufuasi au uwakilishi, wanageukia uchambuzi wa njama za siri.

Viongozi kama Donald Trump pia wanaripotiwa kuchochea nadharia za njama.

Mifano ni pamoja na madai ya Barack Obama kwamba hakuzaliwa Marekani na madai ya Joe Biden kwamba uchaguzi uligubikwa na udanganyifu.

Watu wanaoamini katika nadharia za njama za siri mara nyingi huwa hawaamini vyombo vya habari.

"Wanajikita katika mawazo ya kibaguzi, chuki dhidi ya wageni, na mawazo ya kihafidhina," anasema mtaalamu mmoja.

Inasemekana kuwa Trump alisema kwamba atawakilisha watu ambao "wanatupwa nje" na tabaka la juu.

Kulingana na David Bramwell, mtafiti kuhusu Illuminati, mtu aliyefufua masuala ya Illuminati katika kitabu chake cha miaka ya 1960 "huenda alishangaa na kufurahi" kuona kwamba nadharia ya njama za siri imekuwa maarufu sana.

Wataalamu wanatabiri kwamba kampeni ya kupambana na upotoshaji na ongezeko la harakati za kutilia shaka taarifa zinazochapishwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa siyo za kweli mara zote, itaathiri nadharia za njama za siri kama ya Illuminati.

Asili ya Illuminati

Wazo la asili lilianza zaidi ya miaka 200.

Dada Anna anafanya kazi katika kanisa la Kigothi.

Anajua kwamba watu kutoka Ufaransa, Uingereza, na nchi nyingine huja katika eneo hilo kwa ajili ya "mikutano," lakini hana taarifa wazi kuhusu mahali inapofanyika.

Dada Anna, anayefanya kazi katika duka la vitabu vya kanisa, amesikia kwamba kuna mkutano wa Illuminati huko Bavaria.

Ingawa jiji la Ingolstadt ndilo mahali pakuzaliwa kwa Illuminati, mkutano huo wa siri unaonekana kuwa mbali na ukweli.

Mnamo 1776, Adam Weissput, profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Ingolstadt, alianzisha Illuminati.

Wazo lilikuwa kuunda kikundi cha wasomi wenye uhuru wa kujieleza. Mbali na kundi la ajabu la Freemasons, pia liliathiriwa na wanafalsafa wa Kifaransa.

Ilianzishwa kwa lengo la kuunda kikundi ambapo mawazo huru yanajitokeza, sio kikundi cha kidini.

Haikuwa rahisi kuendeleza mawazo huru katika jiji ambalo mawazo ya kidini yalikuwa yakitawala.

Hapo awali alichagua wanafunzi wake watano waliobobea zaidi kujiunga na kikundi hicho.

Baadae kikundi hiko kiliongezeka haraka.

Wanachama wake walipojaribu kueneza mwanga wa maarifa, walikuwa pia na taarifa za kufuatilia shughuli za serikali na taasisi za kidini.

Walijaribu kueneza mafundisho yao kwa kujikusanyia mali.

Mwanadiplomasia maarufu wa Ujerumani Baron Adolf alikuwa miongoni mwa walioanzisha wazo hilo.

Idadi ya wanachama wake katika Bavaria, Ufaransa, Hungaria, Italia, na Poland ilifikia elfu mbili.

Mwandishi wa habari Michael Kleiner anamwita muundaji wa Illuminati "mwanamapinduzi."

"Alifundisha watu kuwa bora. Alitaka kubadilisha jamii. Alitaka kuona ulimwengu bora na utawala," anasema.

Kinyume na kile kilichoruhusiwa katika chuo kikuu alichofundisha, aliamini kwamba ujuzi wote wa wanadamu unapaswa kutolewa kupitia elimu.

Kundi hilo lilivunjwa lilipokuwa likiendesha harakati za kuipinga serikali katika mwaka wake wa kumi baada ya kuanzishwa kwake, na mwanzilishi wake alikimbilia mji wa Gotha.

Hata hivyo, wanahistoria wanasema bado kuna watu wanaoamini kwamba kundi hilo la ajabu halikupigwa marufuku.

Kulingana na Dk. Michael Wood, anayefanya kazi katika Chuo Kikuu cha Winchester, Illuminati ni nadharia ya njama yenye siri nyingi.

Mji wa Ingolstadt unasemekana kuwa chimbuko la Illuminati.

Kulingana na Maria Ephlischmer, anayefanya kazi katika jumba la makumbusho la jiji hilo, jumba hilo la kumbukumbu lina vitabu vya Illuminati ambavyo vinahusishwa na matukio ya kihistoria ya kuvutia.

Kulingana na Klarner, ambaye hutembelea jiji hilo, hukutana na wageni wanaoamini katika nadharia za njama za siri anapotembelea maeneo muhimu ya kihistoria.

"Jinsi Illuminati inavyoonekana sasa ni ya kushangaza. Inaonekana tofauti sana kuliko Illuminati halisi," anasema.

Sista Anna anasema watu ambao bado wanaamini kuwa mkutano wa Illuminati unafanyika mjini wanamuuliza kuhusu eneo hilo hata kama si kweli.

Kuna wengi wanaoamini kwamba Illuminati ndio inahusika na Mapinduzi ya Ufaransa, shambulio la Septemba 11 dhidi ya Marekani, na matukio mengine muhimu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved