Mawakili wa mgombea urais wa Azimio Raila Odinga tayari wamewasilisha nakala ya kielektroniki ya rufaa ya kupinga ushindi wa Rais Mteule William Ruto.
Timu hiyo ya wanasheria hata hivyo wanatarajiwa kuwasilisha nakala ya rufaa katika mahakama ya Milimani kabla ya saa nane alasiri.
Baadhi ya wanasiasa wa Azimio tayari wamewasili katika mahakama hiyo kwa ajili ya kushuhudia kuwasilishwa kwa rufaa.
Umati wa wafuasi wa muungano huo pia walijitokeza nje ya mahakama ya Milimani Jumatatu asubuhi kumuunga mkono mgombea urais wao.
Baadhi ya wafuasi hao walionekana wakiwa wamebeba mabango ya kudai haki kutendeka.