logo

NOW ON AIR

Listen in Live

CS Magoha: Shule za kutwa katika maeneo uchaguzi kufungwa Agosti 29 (+video)

Shule za bweni hazitafungwa, ikiwa zitatumika kama vituo vya kura, wanafunzi watabaki katika mabweni.

image
na Radio Jambo

Habari23 August 2022 - 09:00

Muhtasari


• Taarifa hii inakuja siku moja tu baada ya tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kutangaza kwamab chaguzi zote zilizoahirishwa zitafanyika Jumatatu Agosti 29.

Waziri wacelimu msomi profesa George Magoha amesema kwamba shule za kutwa katika kaunti za Kaunti za Kakamega na Mombasa pamoja na maeneo mengine ambayo uchaguzi uliahirishwa zitafungwa Agosti 29 na kufunguliwa Agosti 30 ili kupisha tume ya IEBC kutumia sehemu hizo kama vituo vya uchaguzi huo.

Magoha alisema kwamab shule za ndani hazitaathirika na mpango huo kwani wanafunzi watabaki katika mabweni ili kama shule yao ilikuwa moja ya vituo vya kupiga kura, madarasa yatatumiwa kwa shuguli hilo kwa siku hiyo moja na masomo kuendelea kama kawaida kuanzia kesho yake ambayo itakuwa Jumanne Agosti 30.

"Tumekubaliana baada ya kushauriana na Chebukati na Marjani kwamba tutawakubalia kutumia baadhi ya shule kama vituo vya kupiga kura kwa siku hiyo moja (Agosti 29) na pia tumekubaliana kwamba katika maeneo uchaguzi huo utachukua zaidi ya siku moja vituo vyake vihamishwe kwenda maeneo ya masomo ya juu," Magoha alisema.

Alisema kwa sababu hawataki watoto kukosa masomo na kuharibu muda basi watoto watakaokuwa nje kwa hiyo siku moja ni wale wa shule za kutwa na wa shule za ndani watasalia katika mabweni.

"Kwa sababu hatutaki watoto kuharibu muda zaidi, tumekubaliana kwamba shule za ndani hazitafungwa na kama  zinatumika kama vituo vya kura, wanafunzi watabaki katika mabweni na wengine watabaki katika maktaba, wale wa shule za kutwa watabaki nyumbani kwa siku hiyo ya Agosti 29 na kurudi shuleni Jumanne Agosti 30," Magoha alibainisha.

Taarifa hii inakuja siku moja tu baada ya tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kutangaza kwamab chaguzi zote zilizoahirishwa zitafanyika Jumatatu Agosti 29.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved