logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Winnie Odinga: 'Kuwa binti wa Raila ni hasara'

Hata hivyo, alikubali kwamba jina la familia yake pia lilikuwa "baraka" ambayo imemruhusu kusafiri ulimwengu.

image
na Radio Jambo

Habari17 November 2022 - 04:32

Muhtasari


• Bi Odinga alidai kuwa wakosoaji “hawataki kuangazia ninachoweza kufanya” kwa sababu ya babake ni nani.

Winnie Odinga

Winnie Odinga, binti wa kiongozi wa upinzani wa Kenya Raila Odinga, amesema jina lake la familia limemfanya "kunyanyaswa" na "kuteswa" na halikuwa faida ya kisiasa kama wanavyodai baadhi ya wakosoaji.

Winnie Odinga, ambaye anawania kuwa mjumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), alipinga wazo hilo katika kituo cha Citizen TV Kenyakwamba uhusiano wa familia yake ulikuwa nyuma ya uteuzi wake.

Bi Odinga alidai kuwa wakosoaji “hawataki kuangazia ninachoweza kufanya” kwa sababu ya babake ni nani.

Hata hivyo, alikubali kwamba jina la familia yake pia lilikuwa "baraka" ambayo imemruhusu kusafiri ulimwengu na kuelewa jinsi bara la Afrika linaweza kufanya kazi pamoja.

EALA ni chombo cha kutunga sheria cha jumuiya ya kikanda baina ya serikali, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na wanachama wanawakilisha mataifa yao kwa muhula wa miaka mitano.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved