logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rais Ruto akutana na wakurugenzi wakuu wa Safaricom na Vodacom

"Uwekaji wa huduma za serikali katika mfumo wa kidijitali ni kipaumbele cha utawala huu

image

Habari10 January 2023 - 11:30

Muhtasari


  • Rais Ruto alisema anatambua jukumu lililotekelezwa na Safaricom na makampuni mengine ya mawasiliano katika kufanikisha kuanzishwa kwa Hustler Fund

Rais William Ruto Jumanne alikutana na maafisa wakuu kutoka Safaricom Peter Ndegwa na Shameel Joosub wa Vodacom.

Wakurugenzi hao wawili waliandamana na timu zao za usimamizi katika mkutano huo katika Ikulu ya Nairobi.

Rais Ruto alisema anatambua jukumu lililotekelezwa na Safaricom na makampuni mengine ya mawasiliano katika kufanikisha kuanzishwa kwa Hustler Fund.

"Uwekaji wa huduma za serikali katika mfumo wa kidijitali ni kipaumbele cha utawala huu kwa kuzingatia taratibu, utoaji na upashanaji habari," alisema.

"Hii itatufanya kuwa na ufanisi zaidi, kuokoa rasilimali na kuharakisha utekelezaji wa Mpango huo, ambao hatimaye utaboresha ubora wa maisha ya watu wetu."

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved