logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hakuna Maadui wa kudumu kwenye siasa-Kanini Kega asema baada ya kukutana na Rais Ruto

Hakuna maadui wasioweza kusameheana, alitangaza katika hitimisho lake.

image
na Radio Jambo

Makala08 February 2023 - 11:51

Muhtasari


  • Aliendelea kwa kusema kwamba alitembelea Ikulu katika wadhifa wake kama mbunge wa EALA na mkurugenzi wa uchaguzi wa Jubilee

Baadhi ya wabunge wa Jubilee walimtembelea rais William Samoe Ruto katika Ikulu ya Nairobi siku ya  Jumatano.

Wabunge hawa wanaripotiwa kuwa zaidi ya 30. Mmoja wa wabunge hao alikuwa Kanini Kega, mbunge wa bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA).

Kega amejitokeza kutoa taarifa saa chache baada ya mkutano na rais. Mbunge huyo kupitia mtandao wa Facebook alikiri kuwa miongoni mwa wabunge waliomtembelea Ruto. 

Aliongeza kuwa alienda ikulu katika wadhifa wake kama mbunge wa EALA na mkurugenzi wa uchaguzi wa Jubilee.

Mbunge huyo alisema kwamba walikuwa wakumbushana na rais kuhusu maisha yao ya awali wakicheka na walikuwa sasa wameamua kusahau ya kale na kushirikiana.

Hakuna maadui wasioweza kusameheana, alitangaza katika hitimisho lake.

"Tulimtemembelea Rais HE William Ruto na Naibu HE Riggy G katika Ikulu leo. Nilienda huko nikiwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Jubilee na Mbunge wa EALA. Tulicheka mambo yetu ya nyuma na kusameheana na kukubaliana kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya watu wetu. HAKUNA Maadui wa kudumu kwenye siasa!"Alisema Kanini.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved