logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Acheni Upuuzi!' Rais Ruto awaambia Majenerali wa Sudan

Ruto alisema hali hiyo inaangazia mapungufu ya umoja huo.

image
na Radio Jambo

Makala17 May 2023 - 17:18

Muhtasari


  • Pesa zingine zinatoka kwa washirika wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya na mataifa mengine binafsi.

Rais William Ruto Jumatano aliwataka majenerali wanaozozana nchini Sudan "komesheni upuuzi" na kutaka kutafakari upya kwa Umoja wa Afrika (AU) ili kushughulikia vyema mizozo barani humo.

Takriban watu 1,000 wameuawa na karibu milioni moja wamekimbia makazi yao nchini Sudan tangu vita kati ya mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo, anayeongoza kikosi cha wanamgambo kuzuka mwezi Aprili.

"Tunafaa kuwaambia majenerali hao waache upuuzi," Ruto aliambia mkutano wa wabunge wa Afrika nchini Afrika Kusini.

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya dola bilioni 3 (Ksh. 411 bilioni) zitahitajika kutoa msaada wa haraka katika taifa hilo lililokumbwa na mzozo, ambapo mtu mmoja kati ya watatu tayari alitegemea msaada wa kibinadamu kabla ya vita.

Matumaini ya kusitishwa kwa mapigano bado hayajafifia baada ya mapatano mengi kukiukwa katika wiki zilizopita.

Akihutubia katika Mkutano wa Wabunge wa Pan-Afrika, mkutano wa Wabunge wa AU karibu na Johannesburg, Ruto alisema hali hiyo inaangazia mapungufu ya umoja huo.

"Kwa hali ilivyo, hatuna uwezo wa kukomesha upuuzi huu katika bara letu," Ruto alisema, akiongeza kuwa juhudi za amani na usalama za AU zinategemea ufadhili kutoka nje.

"Tunahitaji kutafakari upya Kamati ya Amani na Usalama," alisema, akimaanisha chombo cha AU cha kutatua mizozo.

Nchi wanachama huchangia tu asilimia 37 ya bajeti ya AU, kulingana na ripoti ya umoja huo ya 2021.

Pesa zingine zinatoka kwa washirika wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya na mataifa mengine binafsi.

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved