Waathiriwa wa Shakahola wakulana uroda katika vituo vya uokoaji - DPP

"Waathiriwa sasa wamepona kabisa, wana nguvu na wameripotiwa kufanya tendo la ndoa," Msaidizi mkurugenzi wa DPP aliiambia mahakama.

Muhtasari

• Msaidizi wa mkuugenzi wa mashataka ya umma, alimweleza Hakimu Joe Omide kwamba Serikali inakabiliwa na mzozo mkubwa wa mimba zisizotarajiwa.

• Jamii aliiomba mahakama iamuru wahasiriwa hao wahamishwe kutoka vituo vya uokoaji na kupelekwa katika gereza la Shimo La Tewa.

Image: Screengrab//YouTube

Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma imeelezea hofu kuwa waathiriwa 65 ambao ni mashahidi wakuu katika kesi inayomkabili mhubiri Paul Mackenzie wanajihusisha na ngono katika vituo vya uokoaji.

Msaidizi wa mkuugenzi wa mashataka ya umma, Yamina Jamii, alimweleza Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Shanzu, Joe Omide kwamba Serikali inakabiliwa na changamoto kubwa za mimba zisizotarajiwa na visa vya unyanyasaji wa kijinsia ikiwa waathiriwa wataendelea kuzuiliwa katika kituo cha uokoaji.

"Waathiriwa sasa wamepona kabisa, wana nguvu na wameripotiwa kujamiana. Muda wao mwingi wanautumia kushiriki katika kufanya mapenzi, sambamba na kula na kujumuika kwa uhuru ndani ya vyumba vyao," alisema.

Jamii aliiomba mahakama iamuru wahasiriwa hao wahamishwe kutoka vituo vya uokoaji na kupelekwa katika gereza la Shimo La Tewa ambako watafungwa katika vyumba vya wanaume na wanawake na kusimamiwa kwa urahisi shughuli zao za kila siku.

Mahakama iliambiwa kwamba wawili kati ya walionusurika wana matatizo ya akili, na kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria mara tu familia zao watapatikana.

“Sasa tunaiomba mahakama itowe amri ya kuwapeleka wahasiriwa wote gerezani ili kuepusha mgogoro unaoweza kutokea.

Wahasiriwa hawa waliokolewa kutoka msitu wa Shakahola mwezi Machi mwaka huu baada ya kudaiwa kuingizwa katika dhehebu la mhubiri Mackenzie.

Wakati wakiokolewa, walikuwa wanalazimishwa kufunga ili kuharakisha kifo chao ili waweze kukutana na Yesu.

"Serikali italazimika kushughulikia hata kabla ya kugeuzwa kuwa mashahidi,” alisema.