RIP Shujaa! Rais Ruto amuomboleza shujaa wa Mau Mau, Field Marshall Muthoni Kirima

Rais alimtaja marehemu Muthoni kama mtu mwenye ushawishi mkubwa aliyepigania uhuru wetu.

Muhtasari

•Ruto alitambua ujasiri, uchapa kazi na kutojitolea kwa shujaa huyo aliyeaga wakati wa ukoloni na akamsifu kwa hilo.

•"Tunaheshimu mchango wake wa kishujaa kwa uhuru na maendeleo ya nchi yetu," Ruto alimuomboleza Muthoni.

amemuomboleza marehemu Field Marshall Muthoni.
Rais William Ruto amemuomboleza marehemu Field Marshall Muthoni.
Image: FACEBOOK// GOVERNOR MUTAHI KAHIGA

Rais William Ruto amewaongoza Wakenya katika kuomboleza kifo cha mpigania uhuru Field Marshall Muthoni Kirima aliyeaga dunia Jumatatu usiku.

Katika taarifa yake Jumanne asubuhi, rais alimtaja marehemu Muthoni kama mtu mwenye ushawishi mkubwa aliyepigania uhuru wetu.

Ruto pia alitambua ujasiri, uchapa kazi na kutojitolea kwa shujaa huyo aliyeanguka wakati wa ukoloni na akamsifu kwa hilo.

"Nimehuzunishwa sana na kifo cha Field Marshall Muthoni Kirima, mtu mashuhuri mwenye ushawishi mkubwa ambaye alipigania uhuru wetu," Ruto alisema.

Aliongeza, "Alikuwa jasiri, mchapakazi na aliipenda familia yake, alitumikia jamii yake na alijitolea kwa ajili ya nchi yetu, kila mara kwa bidii kutoka mstari wa mbele. Tunaheshimu mchango wake wa kishujaa kwa uhuru na maendeleo ya nchi yetu na tunamwomba Mwenyezi Mungu aipe familia nguvu katika kipindi hiki kigumu. Pumzika kwa Amani Shujaa wetu.

Muthoni, ambaye alipigana na wakoloni pamoja na marehemu Dedan Kimathi katika milima ya Mt Kenya na Aberdare alikata roho siku ya Jumatatu usiku.

Naibu Rais Rigathi Gachagua alimuomboleza marehemu na kumpongeza kwa ushujaa wake na mchango wake mkubwa katika uhuru wa nchi.

"Nimeamka na habari za kusikitisha za kufariki kwa Field Marshall Muthoni Kirima, mpigania uhuru shupavu ambaye alipigana bega kwa bega na Field Marshall Dedan Kimathi Wachiuri katika misitu ya Mlima Kenya na Aberdare kuwafukuza wakoloni katika ardhi yetu," Gachagua alisema katika taarifa siku ya Jumanne asubuhi.

Aliongeza, "Ninaungana na familia yake na vizazi vya Vita vya Ukombozi vya Mau Mau kuomboleza kifo cha Mama yetu Field Marshall Muthoni wa Kirima."

Gachagua alibainisha kuwa daima Wakenya watakuwa na deni kwa wapigania uhuru kama vile Muthoni kwa juhudi zao kubwa za kuwatimua wakoloni.

Naibu rais aidha aliiombea roho ya marehemu Muthoni ipumzike kwa amani.

"Tunakumbuka kwa fahari na upendo, ushujaa wake katika kuongoza jeshi la ardhi na uhuru baada ya kutekwa kwa shujaa wa uhuru Dedan Kimathi, ambaye alihumu kama msaidizi wake wa kibinafsi, baada ya kusalitiwa na Washiriki. Tunabaki kuwa na deni kwa mashujaa na mashujaa hawa wakubwa kwa mchango wao wa kuikomboa Ardhi yetu. Mungu ampumzishe kwa amani na awape nguvu familia yake iweze kustahimili msiba huo,” alisema.

Muthoni alifariki akiwa na umri wa miaka 92. Roho yake ipumzike kwa amani.