Rais Ruto aomboleza kifo cha mtayarishaji wa wimbo Sipangwingwi

'Wimbo wa sipangwingwi' ilitumiwa na Rais Ruto wakati wa kampeni zake za 2022

Muhtasari

•Rais alisema anakumbuka  hali ya  furaha na utulivu  msanii huyo

• Michango ya Byron katika muziki ilipigiwa upatu wakati wa siasa za 2022 wakati ambapo Rais William Ruto alitumia wimbo huu kujipingia debe
 
 
 

Rais William Ruto ameomboleza kifo mtayarishaji wa muziki wa Gengetone na msanii Byron Kivisi almaarufu Byron Papi.

Kwenye ujumbe wake siku ya Alhamisi, Rais Ruto alisema alihuzunishwa na kifo cha mtaarishaji huyo ambaye alitambulishwa kwake mara ya kwanza wakati wa kurekodi wimbo wa Sipangwingwi.

"Nimehuzunishwa sana na kifo cha mtayarishaji na msanii wa muziki Byron Muhando Kivisi. Byron alitambulishwa kwangu kwa mara ya kwanza na msanii maarufu wa muziki na mwanamuziki Xray wakati wa kipindi cha kurekodi wimbo maarufu wa Sipangwingwi kwenye makazi ya Naibu Rais huko Karen," alisema.

"Inasikitisha kwamba tumempoteza Byron katika umri mdogo. Tunafarijiwa na ukweli kwamba kazi zake za sanaa zitaendelea kuitamba.

Kwa familia, marafiki na mashabiki, pokeeni rambirambi zetu za dhati. Rest In Peace, Byron," Rais Ruto alisema.

Kifo cha ghafla cha Byron Kivisi kilileta mshtuko na kuiacha familia yake na mashabiki katika hali ya huzuni.

Taarifa iliyotolewa na familia yake, ilieleza masikitiko yao makubwa na kutoa maelezo kuhusu chanzo cha kifo chake cha kusikitisha.

Michango ya Kivisi katika  muziki ilitawala chati za muziki na kuingia katika nyanja ya kisiasa. 'Sipangwingwi' ilitumiwa na Rais Ruto wakati wa kampeni zake za 2022.