logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mama alipiwa likizo ya Mombasa kwa kujitolea kumpa malezi bora mwanawe mwenye mahitaji maalum

Mtoto wake,Shujaa ana Celebral Palsy na amekuwa akionyesha mfano mzuri kwa kumpa malezi bora.

image
na Samuel Maina

Habari19 October 2023 - 09:05

Muhtasari


  • •Edinah hatahitaji kujisumbua tena kwani Expendition Maasai Safaris wamejitolea kugharamia kikamilifu safari yao ya siku tatu kwenda Pwani.
  • •Karema alipongeza kujitolea kwa Edinah katika kutoa matunzo bora na usaidizi kwa mtoto wake mwenye mahitaji maalum.

Kampuni ya Expenditions Maasai Safaris imetoa safari ya bure ya siku tatu kwenda Pwani kwa mama ambaye amekuwa akitetea na kuonyesha mfano bora wa malezi bora ya watoto wenye mahitaji maalum.

Edinah Nyamanya alikuwa amemuahidi mwanawe, Shujaa ambaye alizaliwa na hali ya Cerebral Palsy kwamba angempeleka Mombasa mnamo siku yake ya kuzaliwa.

Kufuatia ahadi hiyo, Bi Edinah alikuwa amefanya kazi kwa bidii na baada ya kuweka akiba kwa takribani mwaka mmoja aliweza kukusanya pesa za kumpeleka mwanawe Pwani. Jumatano jioni alikuwa akitafuta mahali ambapo wangelala kwa siku mbili za ziara yao.

“Mwaka huu Shujaa aliniambia, mama nataka unipeleke mahali wakati wa siku yangu ya kuzaliwa na mama akasema ndio baby ngoja nianze kuweka akiba. Kuweka akiba si rahisi, kunahitaji nidhamu kubwa unasota unakumbuka si kuna mahali niko na pesa. Nimekuwa nikiweka akiba Mshwari kidogo kidogo na juu hazitoshi za kununua gari si tuende tufurahie Pwani,” Edinah aliandika kwenye Facebook Jumatano jioni.

Aliendelea kuomba kuelekezwa kwenye hoteli nzuri ambapo yeye na bintiye mwenye mahitaji maalum wangelala kwa siku mbili wiki ijayo.

Edinah hata hivyo hatahitaji kujisumbua tena kwani Expendition Maasai Safaris wamejitolea kugharamia kikamilifu safari yao ya siku tatu kwenda Pwani.

“Tunafuraha kukujulisha kwamba Expeditions Maasai Safaris ina zawadi maalum kwa ajili yako na mtoto wako. Kwa kutambua juhudi zako za ajabu, tunayo heshima kukupa likizo unayostahili. Wewe na mtoto wako ndio mpokeaji wa likizo ya bila malipo ya siku tatu, inayojumuisha kila kitu Mombasa!,” Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Expenditions Safaris Pancras Karema alimwandikia Edinah Alhamisi asubuhi.

Aliongeza, "Tunaamini kuwa upendo wako na nguvu zako zinastahili kusherehekewa, na tunataka kukupa fursa ya kuunda kumbukumbu nzuri pamoja. Timu yetu imejitolea kuhakikisha kuwa kila jambo la safari yako linashughulikiwa, ili uweze kuzingatia kufurahia jua, bahari na mchanga huko Mombasa. Hadithi yako imetutia moyo, na tunasubiri kushiriki katika furaha ya safari yako ijayo. Tunafurahi kuwa sehemu ya sura hii katika maisha yako, na tutafanya kila tuwezalo ili kuifanya tukio lisilosahaulika kabisa.

Karema alipongeza kujitolea kwa Edinah katika kutoa matunzo bora na usaidizi kwa mtoto wake maalum aliye na Celebral Palsy na kumtaka awasiliane na ofisi yao ili kufanya maandalizi ya safari yake ya siku tatu bila malipo.

Edinah anajulikana sana kwa kujitolea kwake katika kutetea malezi bora ya watoto wenye mahitaji maalum. Mtoto wake, ambaye amepea jina Shujaa ana Celebral Palsy na amekuwa akionyesha mfano mzuri kwa kumpa malezi bora.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved