logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahamu kaunti za Kenya ambazo zitakumbwa na mafuriko

MET aliwaonya wakaazi wa kaunti kumi na sita nchini kuwa waangalifu.

image
na Samuel Maina

Habari27 October 2023 - 12:05

Muhtasari


  • •MET ilionya mvua inatarajiwa kuongezeka katika maeneo kadhaa ya Kaskazini Mashariki na Kati mwa Kenya kuanzia Ijumaa, Oktoba 27.
  • •MET aliwaonya wakaazi wa kaunti kumi na sita nchini kuwa waangalifu huku maeneo hayo yakitarajiwa kukumbwa na mvua kubwa.

Idara ya hali ya hewa nchini Kenya imetoa taarifa ya ushauri kuhusu kunyesha kwa mvua kubwa leo, Oktoba 27 na Jumamosi, Oktoba 28.

Katika taarifa ya Alhamisi jioni, watabiri hao wa hali ya hewa walionya kuwa mvua inatarajiwa kuongezeka katika maeneo kadhaa ya Kaskazini Mashariki na Kati mwa Kenya kuanzia Ijumaa, Oktoba 27.

Walitahadharisha kuwa mvua hiyo ingeongezeka zaidi katika maeneo kadhaa ya Kaskazini Mashariki, Nyanda za Juu za eneo la Kati na Pwani ya Kusini kuanzia tarehe 28 Oktoba.

"Mvua hizi huenda zikaambatana na upepo mkali," Met alionya.

Watabiri hao wa hali ya hewa aliwaonya wakaazi wa kaunti kumi na sita nchini kuwa waangalifu huku maeneo hayo yakitarajiwa kukumbwa na mvua kubwa.

Walitahadharisha kuwa kaunti za Marsabit, Mandera, Wajir, Garissa, Isiolo, Embu, Nyeri, Meru, Kiambu, Nyandarua, Laikipia, Murang’a, Kirinyaga, Tharaka Nithi, Kwale na Mombasa huenda zikakumbwa na mafuriko na kuwaonya wakazi kuwa waangalifu.

"Maji ya mafuriko yanaweza kutokea katika maeneo ambayo mvua haijanyesha hasa chini ya mto. Wakaaji wanashauriwa kuepuka kuendesha gari, au kutembea kwenye maji yanayosonga au uwanja wazi na kutojificha chini ya miti na karibu na madirisha yaliyochomwa wakati wa mvua ili kupunguza uwezekano wa kupigwa na radi. Upepo mkali unaweza kuvuma paa zako, kung’oa miti na kusababisha uharibifu wa miundo,” MET ilisema.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa ilisema kwamba watatoa sasisho iwapo kuna mabadiliko yoyote au maendeleo katika utabiri wa hali ya hewa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved