logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamke akamatwa kwa kifo cha mtoto wake wa miaka 10 Trans Nzoia

Hii itaamua sababu ya kifo na hatua ya mama huyo, polisi walisema.

image
na Radio Jambo

Habari29 October 2023 - 10:01

Muhtasari


  • Kifo hicho kilitokea katika eneo la Pileland katika Kaunti Ndogo ya Trans Nzoi Magharibi, polisi walisema.

Polisi wanamshikilia mama mwenye umri wa miaka 25 kutokana na kifo cha mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 10 baada ya kudaiwa kumpiga.

Kifo hicho kilitokea katika eneo la Pileland katika Kaunti Ndogo ya Trans Nzoi Magharibi, polisi walisema.

Mwanamke huyo aliripoti katika kituo cha polisi cha Saboti mnamo Jumamosi, Oktoba 28, 2023 asubuhi, akisema kwamba alimpata mwanawe akiwa amefariki alipoamka.

Aliwaambia maafisa kwamba mvulana huyo alitoweka nyumbani hapo awali na aliporudi, alimpiga kwa fimbo ili kumtia nidhamu.

Baada ya kupigwa viboko, mwanamke huyo na mwanawe waliendelea kula chakula cha jioni na kwenda kulala.

Hata hivyo, alipozinduka, mwanamke huyo alisema alimkuta akiwa amelala chini bila kuitikia.

Polisi walizuru eneo la uhalifu na kuuhamisha mwili wa marehemu hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Kitale kusubiri zoezi la uchunguzi wa maiti.

Hii itaamua sababu ya kifo na hatua ya mama huyo, polisi walisema.

Misiba kama hii ambapo watoto hufa baada ya kipigo inaongezeka. Viongozi wanahimiza tahadhari miongoni mwa wazazi na walezi.

Wakati huo huo, polisi katika kijiji cha Gichagi II huko Ithanga Kakuzi, Kaunti ya Murang'a, wanamsaka mwanamke mwenye umri wa miaka 53 kwa madai ya kumpiga mwanawe hadi kumuua kufuatia ugomvi kati ya wawili hao usiku wa Oktoba 21, 2023.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved