logo

NOW ON AIR

Listen in Live

RIP: Mwimbaji wa bendi ya Jacob Luseno katika kibao maarufu 'Mukangala' afariki dunia

Anyika alifariki akipokea matibabu katika hospitali ya Moi jijini Eldoret.

image
na Radio Jambo

Habari17 December 2023 - 09:06

Muhtasari


• Anyika ni sauti maarufu ya kike katika Bendi ya Phonotex Success, iliyoanzishwa na marehemu Jacob Luseno mnamo 1965.

• Alirekodi nyimbo nyingi zilizovuma akiwa na Luseno. Wimbo maarufu zaidi ni Mukangala na Amakuru, uliorekodiwa mwaka wa 1974.

Mwimbaji wa Jacob Luseno.

Wapenzi wa nyimbo za kutoka ukanda wa Magharibi wa Kenya wametupwa kweney kipindi cha maombolezo kufuatia kifo cha msanii wa bendi ya Phonotex ambayo inaongozwa na msanii maarufu Jacob Luseno.

Gertrude Mwendo Anyika, ambaye alifahamika na wengi kwa sauti yake ya kuvutia katika kibao maarufu kwa jina ‘Mukangala’ alitangazwa kufariki usiku wa kuamkia Desemba 17 baada ya muda mrefu wa kupambana na saratani, taarifa zilisema.

Anyika alifariki akipokea matibabu katika hospitali ya Moi jijini Eldoret.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mwanablogu Mwalimu Amunga Akhanyalabandu alithibitisha kifo cha Anyika mnamo Ijumaa, Desemba 15.

"Gertrude amekuwa hospitalini kwa miezi kadhaa akiugua saratani. Bili zake kubwa zilikuwa KSh 2.5 milioni, ambazo familia haikuweza kulipa. Alikuwa katika wadi ya umma. Hospitali ya Kufundisha na Rufaa ya Moi huko Eldoret," Amunga alichapisha kwenye X.

Anyika ni sauti maarufu ya kike katika Bendi ya Phonotex Success, iliyoanzishwa na marehemu Jacob Luseno mnamo 1965.

Alirekodi nyimbo nyingi zilizovuma akiwa na Luseno. Wimbo maarufu zaidi ni Mukangala na Amakuru, uliorekodiwa mwaka wa 1974.

Nyimbo nyingine ni pamoja na Injeti, Masiali, Cecilia, Regina, House Maid, Bushuma Bwa Malika, Ingato, na Linda, miongoni mwa nyimbo zingine


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved